Friday, October 17, 2014

SIMBACHAWENE AAGIZA WATENDAJI KULINDA MAENEO YA WAZI

1aNaibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. George Simbachawene akizungumza na viongozi na watendaji wa Manispaa tatu za Jiji la Dar es Salaam kuhusu maagizo ya namna ya kusimamia maeneo ya wazi. Pia, ametoa siku 14 kuanzia leo kwa Manispaa hizo kubomoa maeneo ya wazi yaliyovamiwa ambayo yalikwishatolewa Ilani. Aidha, Naibu Waziri ametoa siku 30 kwa Manispaa ya Kinondoni kuwasilisha ofisini kwake utaratibu wa namna ya kusafisha fukwe.(Picha zote na Rehema Isango)
2Watendaji wa Manispaa zote tatu za Jiji la Dar es Salaam pamoja na wataalam wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. George Simbachawene kuhusu namna yak usimamia maeneo ya wazi jijini Dar.
3Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. George Simbachawene (katikati) akitoa maagizo ya usimamizi wa maeneo ya wazi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meya wa Manispaa ya Temeke Bw. Maabad Hoja na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Bw. Khery Kessy.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...