Friday, October 17, 2014

NHC yaelezea namna ilivyosaidia vijana kupitia mradi wa ufyatuaji wa matofali na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu

 Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo,  akimpa maelezo ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu Mkuu wa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Bi Susan Omari alipotembelea mradi huo ulioko eneo la Isikizya Wilayani Uyui jana.
 Mwonekanao wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Isikizya Mkoani Tabora.
 Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akiendelea kutoa maelezo ya mradi kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Bi Susan Omari
 Nyumba 38 zilizojengwa karibu kabisa na Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui eneo la Isikizya. Nyumba zingine 12 zimejengwa upande wa pili wa barabara eneo la Isikizya.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Chilambo
 Msimamizi wa mradi wa NHC isikizya Bw. Tokimu Mondo akitoa maelezo ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu eneo la Isikizya jana.
 Sehemu ya nyumba zilizojengwa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu eneo la Isikizya Wilayani Uyui zinavyoonekana.
 Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Chilambo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Bi. Susan Omari yanayohusu viwanja vya Shirika vilivyoko eneo la Itetemia Manispaa ya Tabora.
 Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akielezea hatua mbalimbali zilifikiwa na Mkoa huo za kutengeneza nyumba za Shirika. Hili ni mojawapo ya jengo la Hoteli ya Golden Eagle baada ya kufanyiwa matengenezo.
 Sehemu ya mtaa wa Jamhuri/Shule wenye nyumba zilizofanyiwa matengenezo makubwa na NHC Mkoa wa Tabora
 Mojawapo wa jengo lililofanyiwa matengenezo na NHC Mkoa wa Tabora linavyoonekana kwa sasa
Sehemu ya Maafisa Vijana wakisikiliza mada iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari (hayuko pichani) alipoelezea mpango wa NHC wa kugawa mashine kwa ajili ya kusaidia vijana kwenye Halmashauri zote za Wilaya hapa nchini. Jumla ya mashine 656 zimeshambazwa kwa ajili hiyo.
 Washiriki wa semina iliyotolewa na NHC wakisikiliza mada kwa makini
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari akitoa mada juu ya mpango wa NHC wa kusaidia vijana mashine za kufyatulia matofali katika Halmashauri zote za  Wilaya nchini.
 Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akilishukuru Shirika la Nyumba la Taifa kwa uamuzi wake wa kizalendo wa kusaidia vijana mashine ili waweze kujiajiri alipochangia mada iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC.
Katibu  Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, , Bibi Sihaba Nkinga akitoa maelezo wakati wa semina iliyotolewa na NHC mjini Tabora jana.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...