Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim akipokea Tuzo ya Juu ya Umoja wa Afrika ya Mwana wa Afrika kwa Mwaka 2014 kutoka kwa Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika, Mhe. Balozi Smail Chergui. Tuzo hiyo ilitolewa mjini Arusha pembezoni mwa Warsha ya Tano ya Ngazi ya Juu kuhusu Amani na Usalama Bararani Afrika iliyoandaliwa na Umoja wa Afrika inayoendelea mjini humo.
Tuzo hiyo pia imetolewa kwa Balozi Mstaafu na Mpigania Uhuru Mahiri Barani Afrika, Balozi Hashim Mbita. Tuzo hizo zimetolewa kwao kutokana na mchango mkubwa walioutoa Barani Afrika na kwa Umoja wa Afrika ambapo Dkt. Salim alikuwa Katibu Mkuu wa saba wa OAU kuanzia mwaka 1989 hadi 2001. Kwa upande wake Balozi Mbita alikuwa Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Ukombozi Barani Afrika chini ya OAU kuanzia mwaka 1974 hadi 1994 ilipomaliza kazi yake baada ya Uhuru wa Afrika Kusini.
Balozi Chergui akimkabidhi Cheti cha Tuzo hiyo Dkt. Salim |
Dkt. Salim akipongezwa na Balozi Chergui |
Balozi Chergui akimkabidhi Cheti Bi. Sheila Hashim Mbita kwa niaba ya Balozi Mbita |
Balozi Chergui akimpongeza Bi. Sheila Hashim Mbitaaliyepokea Tuzo kwa kwa niaba ya Balozi Mbita |
Dkt. Salim akipongezwa na Balozi Augustine Mahiga huku Rais Mstaafu wa Cape Verde (kulia) akushuhudia. |
Dkt. Salim akipongezwa na wajumbe mbalimbali waliokuwepo wakati wa hafala ya utoaji Tuzo. |
Dkt. Salim katika picha ya pamoja na Balozi Naimi Aziz |
Dkt. Salim katika picha ya pamoja na Bi. Zuhura Bundala, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. |
Balozi Aziz katika picha ya pamoja na Bi. Sheila Mbita |
Balozi Aziz akiwa na Balozi Mahiga katika picha ya pamoja na Bi. Sheila Mbita. |
No comments:
Post a Comment