Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika(MISATAN) Bwana Andrew Marawiti akizungumza jambo wakati akifungua kongamano na maafisa habari wa taasisi za serikali zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.
********************************************
Na Mwandishi wetu
Maafisa habari mbalimbali kutoka wizara na mihimili tofauti ya nchi, jana walikutana katika hoteli ya JB Belmont hapa Dar es Salaam kujadili changamoto wanazo kumbana nazo wakati kwa kutoa taarifa kwa wananchi.
Kongamano hilo linafuatia matokeo ya utafiti wa upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) nakuzinduliwa rasmi siku ya tarehe 28 Septemba, ambayo pia ni Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa.
Miongoni mwa taasisi zilizoshiriki katika kongamano hilo ni Bunge, Mahakama, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Nishati na Madini, Idara ya Habari Maelezo, Mamlaka ya Taifa ya Vitambulisho (NIDA) na Idara ya Taifa ya Takwimu. Wizara za Afya na Mambo ya Nje hazikuweza kuwakilishwa licha ya kupata mwaliko.
Mwanasheria kutoka Taasisi Kitaifa ya Msaada wa Kisheria (National Organization of Legal Assistance-nola) Bwana James Malenga akisisitiza jambo alipokuwa anawasilisha mada yake kwenye kongamano hilo la maafisa habari wa taasisi za kiserikali lililoandaliwa na Misa-Tanzania.
Afisa Habari na Utafiti wa Misa-TanzaniaBwana Sengiyumva Gasirigwa akitoa ufafanuzi kwenye mada aliyokuwa anaiwasilisha kwenye kongamano la maafisa habari wa taasisi za kiserikali (hawapo picha)
Mfanyakazi wa Misa-TanzaniaBwana Idrisa Abdallah akizungumzia adha anazozipata anapokuwa anakwenda taasisi na idara mbalimbali za serikali kupeleka barua ama maombi ya taarifa.
Afisa habari wa Mahakama Bi. Mary C. Gwera akizungumza jinsi ofisi yake ilivyopokea Tuzo ya Kufuli na ambavyo imekuwa chachu ya mabadiliko katika kutoa taarifa kwa umma.
Afisa Mwandamizi wa habari kutoka Idara ya Habari Maelezo Bwana Abraham Nyantori akielezea changamoto za utoaji taarifa katika taasisi na idara za serikali.
Maafisa habari wakifuatilia kwa umakini mada ya Umuhimu wa Kutoa kupata Taarifa serikalini kutoka kwa mwanasheria wa kujitegemea Bwana James Marenga.
Kaimu Mkurugenzi wa Misa-Tanzania Bwana Andrew Marawiti akitoa shukrani wa wageni waliofika kwenye kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment