Wednesday, October 15, 2014

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki Atembelea Eneo La Mbagala Rangi 3 Lilopinduka Lori la Mafuta na Kulipuka na Kusababisha Vifo Vya Watu wa 3 na wengine 16 Kujeruhiwa


  Lori hilo lilivyoteketea kwa moto uliosababishwa na mshumaa.
 Moja ya maduka ya vifaa vya pikipiki lililoteketea

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiangalia tenki la lori hilo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema wakimsikiliza miliki wa Nyumba ya kulala wageni United State na bar, Laurent Kasiga  iliyopo Mbagala Rangi tatu, Dar es Salaam ambayo iliteketea kwa moto uliotokana na roli la mafuta lililopinduka na kuwaka moto wakati vijana wakiiba mafuta.
  Mkuu wa Mkoa akikagua Nyumba hiyo ya kulala wageni iliyokuwa na vyumba 32.
 Wafanyabiashara wa mchele waliokuwa na fremu katika eneo hilo wakiwa katika majonzi baada ya mzigo wao kuungua moto na kuharibika kabisa

BOFYA HAPO CHINI KUMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MECK SADIKI AKIZUNGUNZIA TUKIO HILI PAMOJA NA BAADHI YA MASHUHUDA

  Wananchi wakiangalia athari za moto huo.
WATU wa tatu wamefariki dunia huku wengine 16 wakijeruhiwa katika ajali ya lori la mafuta lililopinduka katika mzunguko wa Mbagala Rangi tatu jijini Dar es Salaa jana usiku. 

 Ajali hiyo ya lori la mafuta ilitokea wakati lori hilo ambalo halijafahamika ni mali ya kampuni gani kupinduka wakati dereva wake akijaribu kulikwepa gari lingine lililokuwa mbele yake. Akisimulia chanzo cha ajali hiyo mmoja wa mashuda amesema mara baada ya gari hilo kupinduka dereva alitoa tahadhari kwa vijana waliofika eneo hilo kuwa waache kuchota mafuta hayo na endapo wakifanya hivyo wathithubutu kuwasha moto au kugusa betri lakini ghafla palitokea mtu aliyewasha mshumaa jirani.

 Kuwashwa kwa mshumaa huo kulisababisha moto kulipuka na hatimaye moto kufika hadi katika gari hilo na kuunguza watu waliokuwa wakichota mafuta. Mmoja wa waliokuwa wakichota mafuta alikimbilia baa ya United State kutafuta maji ajizime moto na kusababisha moto kulipuka tena eneo hilo la bar na mtu mwingine alikimbilia eneo la gesti kutafuta maji nae akasababisha moto katika magodoro na kuiteketeza kabisa nyumba hiyo ya wageni iliyo na vymba 32. 

Mbali na nyumba hiyo ya wageni pia moto huo uliteketeza kabisa mali katika vibanda vinne vya biashara vilivyokuwa eneo hilo na pikipiki. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic alifika katika eneio la tukio na kutoa onyo kwa wananchi kusogelea magari ya mafuta yanapo anguka.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...