Washiriki wa kongamano lamafunzo ya mfumo mpya wa shirika la kimataifa la usafiri wa anga (ICAO)kutoka nchi za Nigeria,Mali,Ivort coast,Senager,Rwanda,Cape Verde,Gabon na Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Kongamano hilo la siku tatu linalofabnyika kwenye hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Kanda ya Afrika wa ICAO Papa Issa Mbengue (kushoto)akisisitiza jambo juu ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye kulenga ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege wakati wa Kongamano la mafunzo ya ufanisi wa masuala ya uongozaji wa ndege linalofanyika kwa siku tatu katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wanaomsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha(watatu kutoka kulia) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma za Uongozaji ndege Said Onga (Kulia) Meneja mratibu wa safari za ndege Afrika Frederic Legrand. (wapilia kutoka kulia) na Makamu wa rais wa airspace and airlines Servises Airbus ya Ufaransa Don Facpues
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha akisalimiana na baadhi ya washitiki wa kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye ufanisi wa wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege,wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa hapo kongamano hilo limedhaminiwa na TCAA linalofanyika kwa siku tatu kuanzia jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha (kulia)akisalimiana na Makamu wa rais wa airspace and airlines Servises Airbus ya Ufaransa Don Facpues Ould, baada ya kufungua kongamano la mafunzo ya mfumo mpya wa shirika la Kimataifa la usafiri wa Anga (ICAO) lenye ufanisi wa kulenga wataalamu wa kuongoza ndege ,vyombo vya usafiri wa anga pamoja na mitambo ya kuongonzea ndege.Kongamano hilo linafanyika kwa siku tatu kuanzia jana katika hateli ya Serena jijini Dar es Salaam.Katikati ni Meneja mratibu wa safari za ndege Afrika Frederic Legrand.(African Flight Proceducare Manager)
No comments:
Post a Comment