Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara Mhe. Mark Mwandosya
akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kenya Mhe William Ruto wakati wa
sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka juzi.
Mhe. Mwandosya alimuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe
hizo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara Mhe. Mark Mwandosya (wa
tatu kulia ) pamoja na Mkewe Lucy Mwandosya wakishiriki kuimba Wimbo wa
Taifa wa Zambia wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa
Zambia Mjini Lusaka juzi. Wengine kutoka kulia ni Kaimu Rais wa Zambia
Mhe Edgar Lungu ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi, na wa pili kulia ni
Makamu wa Rais wa Nigeria Monance Namadi Sambo.
No comments:
Post a Comment