Thursday, October 30, 2014

SERIKALI YAAHIDI KUTAFUTA UFUMBUZI SUALA UHABA WA MAGHALA

…………………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
Waziri Mkuu Mizengo  Pinda amesema  Serikali imeanza kulifanyia kazi tatizo la wakulima kukosa mahali pa kuhifadhia ya mazao yao, hivyo  litapatiwa  ufumbuzi katika kipindi cha miezi mitatu hadi minne ijayo baada ya mpango wa kujenga maghala makubwa kuanza.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu, Pinda  katika mkutano wake na waandishi wa habari alioufanya mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu  Julius  K.Nyerere  uliopo jijini Dares Salaam kufuatia ya ziara yake ya kikazi katika nchi za Uingereza, Poland na Oman. yenye lengo la kuhimarisha mahusiano.
Waziri Mkuu Pinda alisema ametembelea nchi ya Poland, ambayo ilikuwa na lengo la kuhimarisha mahusiano na ushirikiano na kutafuta msaada wa mfumo wa mkopo wenye masharti nafuu wa kusaidia kupambana na tatizo la uhaba wa maghala  kwa ajili ya kuhifadhia nafaka au chakula.
Alisema katika nchi hiyo amejionea jinsi ilivyo kuwa na mfumo  maalum  wenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi chakula.
“Unahitajika mfumo huu wa Poland wenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi  chakula. Hivyo tunahitaji kiasi cha fedha cha  Sh.  bilioni 240 hadi  bilioni 260  kwa ajili ya kukabilian na tatizo hili, tumeandika ombi na tumeshapeleka  kwa Serikali,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
 Aliongeza kwamba  pia wameomba mkopo wenye masharti nafuu ili kusaidia kupambana na tatizo la uhaba wa maghala kwa ajili ya kuhifadhia chakula, hivyo kwa kuanzia wameomba mkopo wa Euro milioni 500 katika nchi ya Poland,ambao wenye riba  nafuu ya kiasi cha 0.25.
 Alisema lengo ni kujenga maghala kubwa katika  baadhi ya mikoa, ambayo aliitaja kuwa ni  Rukwa, Ruvuma, Iringa, Njombe, Dodoma,  Tanga na ghala dogo katika  Kanda ya Ziwa.
Akizungumzia kuhusu uzalishaji wa mahindi nchini alisema wakulima wameweza kuzalisha tani 500,000 za mahindi, lakini changamoto iliyopo iliyopo   ni mahali pa kuhifadhia.
 Aliongeza kuwa uwezo wa maghala ya  Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula(NFRA) ni tani 240,000  wakati bado kuna tani zaidi ya 200,000 zilizozalishwa mwaka jana (msimu uliopita) za mahindi na katika kipindi cha sasa wamepanga kununua  tani 3.
Waziri Mkuu Pinda alisema Serikali imeshirkisha sekta  binafsi ili iweze kununua tani 200,000 na lakini bado chakula ni kipo cha kutosha.
 Alisema kwa upande wa mpunga kuna tani zaida 800,000 kwani msimu huu zilimezalishwa tani milioni 1.5. hali hiyo imechangiwa na matumizi ya mbegu bora, mbolea na  matumizi ya matrekta.
Waziri Mkuu aliwapongeza wakulima kwa juhudi zao za kulizalisha chukula cha kutosha.
Akizungumzia kuhusu ziara yake nchini Oman alisema ilikuwa na lengo la kuhimarisha mahusiano na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara.
Alisema nchi hiyo mwikitio wa nchi hiyo wa kuwekeza ni mzuri hususan kwenye kilimo, mifugo na uvuvi.
“ Eneo walioonesha hisia ni la mifugo,  hasa

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...