Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, hupata fursa ya kujionea na kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo kujua fursa ya kujipatia mikopo ya nyumba kama huyu (Kushoto), aliyetembelea banda la PSPF lililoko kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini
Afisa wa PSPF, (Kushoto), akimpatia maelzo ya kina mwanachama huyu aliyefika kwenye banda hilo
Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, (Kushoto), akiuliza maswali huku Afisa Masoko wa Mfuko huo, Bi. Rahma, akimsikiliza kwa makini, wakati alipotembelea banda la PSPF, lililo kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, viwanja vya Mwalimu Nyerere, jijini
Mfuko wa Pensheni wa PSPF, hutoa huduma kwa wanachama wake kwa njia mbalimbali ikiwemo ile ya "Kiosk", ambapo bila shaka Mwanachama huyu (Kulia), alihitaji kujua utendaji kazi wake, na hapa anapatiwa maelezo ya klutosha
Afisa nmwandamizi anayeshughulikia mifumo ya taarifa na elektroniki wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Mariam Saleh (Kulia), akijadiliana jambo na maafisa wengine wa Mfuko huo juu ya namna bora ya kutoa huduma kwa wanachama na wananchi wanaotembelea banda la PSPF kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba
No comments:
Post a Comment