Rais wa Jamhuri ya Sierra Leone, Mheshimiwa Julius Maada Bio, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaotarajiwa kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kuanzia tarehe 27 hadi 28 Januari 2025.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mheshimiwa Rais Bio amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo.
Mheshimiwa Rais Bio ni Rais wa kwanza kuwasili nchini kwa ajili ya mkutano huo ambao jumla ya Marais 25 kutoka nchi za Afrika aanatarajiwa kuja nchini kushiriki mkutano huo.
Mkutano huu wa kihistoria unalenga kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto na fursa za nishati barani Afrika, sambamba na kupitisha Azimio la Dar es Salaam, linalosisitiza dhamira ya Viongozi wa Nchi na Serikali za Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu barani Afrika.
No comments:
Post a Comment