Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw. Peter Ngota na baadhi ya maofisa wa kampuni hiyo wakiwa katika hafla hiyo
Kaimu Mkuu wa Fedha Alinanuswe Mwakitalima akitizama tuzo baada ya kushinda katika Maonesho ya Biashara
………………………………………………………………………..
KAMPUNI ya Simu Tanzania, TTCL imeshinda tuzo katika kundi la kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano, kwenye Maonesho ya 38 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. Makamy wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu, Peter Ngota katika uzinduzi rasmi wa Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Ushindi wa TTCL unatokana na ubora wa huduma zinazotolewa na kampuni hiyo katika upande wa mawasiliano ya simu na pia mawasiliano ya intaneti “DATA”. TTCL imesema ushindi huo umeipa hamasa ya kuendelea kubuni bidhaa ambazo zitakuwa chachu ya ukuaji uchumi nchini.

No comments:
Post a Comment