Thursday, July 02, 2015

WANAWAKE WATAKIWA KUJIAMINI KATIKA NAFAZI ZAO ZA UONGOZI -KAIRUKI

 Katibu mtendaji wa uongozi institue,Profesa Joseph Semboja  akizungumza katika mkutano wa kuwajengea uwezo wanawake katika masuala ya uongozi uliofanyika katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanawake walioshiriki mkutano wa kuwajengea uwezo katika masuala ya uongozi uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Nabu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Angela Kairuki akizungumza na wanawake katika mkutano wa kuwajengea uwezo wanawake katika masuala ya uongozi uliofanyika katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
NAIBU  Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Angela Kairuki amewataka wanawake kujiamini katika nafasi za uongozi wanazozipata katika kuweza kufikia asilimia ya 50 kwa 50.
Hayo aliyasema katika mkutano wa wanawake ulioandaliwa na uongozi Instute,Kairuki amesema katika kuelekea katika uchaguzi mkuu wanawake wajitokeze katika nafasi mbalimbali ili kuweza kubadilika.
Amesema katika ngazi mbalimbali za maamuzi katika bodi zilizopo nchini ni idadi ndogo za wanawake ikilinganishwa na wanaume hali ambayo sasa inatakiwa kuweka kupaumbele katika bodi kuwa na uwakilishi wa wanawake.
Kairuki amesema sasa ni wakati wa mabadliko kwa wanawake kuonyesha uwezo katika kazi mbalimbali na kujenga mazingira ya kujiamini katika kazi iwe  nafasi za ukurugenzi na kazi nyinginezo za serikali na sekta binafsi.
Nae Katibu Mtendaji wa Uongozi Institute,Profesa Joseph Semboja amesema wameanza program hiyo katika kuwainua wanawake katika nafasi za uongozi katika kuweza kufikia malengo ya asilimia 50 kwa 50.
Sembomja amesema wanawake katika kuelekea uchaguzi mkuu ni fursa kwao kujitokeza kutokana na mafunzo mbalimbali wanayopata kutoka kwa wanawake waliokatika nafazi za uongozi.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...