MWANDISHI wa habari mkongwe, ambaye amejishindia tuzo mbalimbali ikiwemo ile ya CNN, Richard Mgamba, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The Guardian Limited, na tayari amekwisha kabidhiwa "mikoba" na aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo, Bi.oyce Mhavile, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One. Mhavile alikuwa kikaimu nafasi hiyo, baada ya
aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wake, Kiondo Mshana, kustaafu kwa mujibu wa sheria. Mara ya mwisho Mgamba akikjuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Citizen. Pichani Mgamba, akionyesha alama ya dole, ikiwa ni ishara ya ushindi, baada ya kunyakua tuzo ya CNN mwaka 2008
No comments:
Post a Comment