Friday, July 03, 2015

NHC YANYANG’ANYA MASHINE ZA KUFYATULIA MATOFARI BAADA YA HALMASHAURI ZA MIKOA BAADA YA KUSHINDWA KUTUMIA FURSA HIYO

● Mkoa wa Katavi na Rukwa washindwa kutumia fursa ya msaada huo
● NHC yanyang’anya mashine Halmashauri za Mikoa hiyo
● Zatakiwa kuomba upya mashine hizo na kuunda vikundi imara
Katika kuhakikisha kuwa rasilimali za umma zinatunzwa, kutumika ipasavyo na kuhakikiwa, NHC imeendelea kuwakagua vijana waliopewa msaada wa mashine za kufyatulia matofali yatakayowezesha wananchi kujijengea nyumba za gharama nafuu katika Halmashauri zote za Mikoa ya Katavi, Mbeya na kukamilika Mkoani Iringa. Kwa ujumla, vijana wana ari ya kutosha ingawa wana changamoto zinazohitaji msukumo wa Halmashauri zao, hasa za masoko ya matofali yao pamoja na mtaji wa kuwawezesha kuendelea na uzalishaji wa benki ya matofali ya kuuzia wananchi. Katika ziara ya NHC Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya hizo wameomba NHC isiwanyang’anye mashine na wameahidi kuwapa vijana mikopo na kuwasaidia malighafi za kuwawezesha kutengezea matofali hayo ikiwemo mchanga, sementi na udongo maalum kwa kazi hiyo. Hata hivyo, Mikoa ya Rukwa na Katavi muitikio wa vijana na Halmashauri hizo ukiacha Halmashauri ya Mlele ambayo inafanya vizuri, umekuwa hafifu sana na Shirika limelazimika kuzinyang’anya Halmashauri hizo mashine na kuzitaka kuomba upya kama bado wana azma ya kutumia mashine hizo kujiletea maendeleo ya kuwa na nyumba bora na kukuza ajira kwa vijana wao. Fuatilia yaliyojiri katika uhakiki huo katika picha.
New Picture (1)

Kikundi cha ‘Mshikamano’ katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kikimsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC BW. Muungano Saguya akiwaelezea namna ya kukuza ujuzi na kutumia Halmashauri zao kuongeza ufanisi wa kazi alipowatembelea nakusaidia  kuondoa changamoto zinazowakabili. Vijana hao wameshapewe  eneo la muda la kuendesheea shughuli zao na wameanza kutengeneza tofali kwa ajili ya kuwauzia wanmanchi.
New Picture (2)
Hii ndiyo hali iliyojitokeza Mkoani  Katavi katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda pale NHC ilipolazimika kuzitwaa mashine ilizotoa msaada kwa vijana ili waweze kujiajiri. Kikundi hiki cha Mpanda Hotel ni mojawapo ya vikundi vilivyonyang’anywa mashine Mkoani Katavi na Rukwa kwa Halmashauri sita za Mikoa hiyo ukiacha Mlele inayofanya vizuri, kushindwa kuzitumia mashine hizo ipasavyo. Halmashauri hizo zimetakiwa kuomba upya mashine hizo na kuunda vikundi imara baada ya kubainika kuwa vikundi vya awali  vilundwa kisiiasa.
New Picture (3)
Kikundi cha vijana cha ITIMBA kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini  kikimsikiliza` Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Kasibi Saguya  alipowatembelea ili kujuwa changamoto zinazowakabili. Kikundi hicho kimeshapata kazi za watu binafsi na shule ili kuwajengea majengo mbalimbalia na hivyo kupata fedha za kujiendeleza. Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini imekubali kuwapa vijana hao ardhi na maeneo ya kufanyia kazi.
New Picture (4)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri ya Wilaya ya  Ileje Bw. James Milanzi  akimsikilza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipofika Ofisini kwake kukumbusha wajibu wa Halmashauri za Wilaya wa kusaidia vijana ili waweze kutengeneza matofali ya kujengea nyumba za gharama nafuu na kujipatia ajira. Halmashauri hiyo imepiga marufuku ukataji miti kwa ajili ya kuchoma matofali na badala yake wananchi wametakiwa kutumia matofali rafiki wa mazingira yanayozalishwa kwa kutumia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana katika Halmashauri zote nchini.
New Picture (5)
Kikundi c ha “CHAPAKAZI” Wilayani  Mbarali kikiwa  kinamsikiliza  Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipowatembelea kujuwa changamoto zinazowakabili.Halmashauri ya Mbarali imesaidia vijana vifaa na maeneo ya kutengenezea matofali hayo na vijana wamehamasika baada ya kuhakikishiwa soko la tofali zao.
New Picture (6)
Kikundi cha “JITEGEMEE NA CALVARY “ Wilayani Tukuyu kikiwa tayari  kumsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamiii wa NHC Bw. Muungano Saguya alipowatembelea ili  kujuwa changamoto zinazowakabili. Kikundi hicho kimeishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Tukuyu  kwa kuwapa eneo la kufanyia kazi na masoko ya tofali wanazatengeneza. Kushoto ni Meneja wa NHC Mkoa wa Mbeya Bw. Anthony Komba.
New Picture (7)
Kaimu Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi  Bw. Ubisimbali Jesiwande alipokutana na timu ya NHC na kuchangia hoja ya  namna ya kuondoa changamoto za ajira zinazowakabili vijana nchini. Halmashauri hiyo ambayo vijana wake hawajafanya vizuri imeapa kuwapa vijana wake mikopo na kuwatafutia masoko ya matofali yao.
New Picture (8)
Kikundi cha “Umoja wa matofali imara” Wilayani Iringa Vijijini ambacho kimeshajenga jengo kubwa la kibiashara kwa kutumia mashine kilichopewa msaada na NHC kilipata fursa ya kutembelewa na ujumbe kutoka NHC na kupewa msasa na hamasa ya kuendelea kujiletea maendeleo kwa kutumia mashine hizo.
New Picture (9)
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Bi. Sikitu Mwemsi (kulia) akiomba timu ya NHC iliyofanya mazungumzo naye Ofisini kwake kuwapa muda badala ya kuwanyang’anya mashine walizopewa baada ya Halmashauri hiyo kususua kuwasaidia vijana na kusimamia vikundi vyao. Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC ameipa Halmashauri hiyo mwezi mmoja kujiweka sawa na vijana wake kuanza kutumia kikamilifu mashine walizopewa msaada na NHC. 
New Picture (10)
Timu ya NHC na Maofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo ikiwa eneo linalotumiwa na kikundi cha vijana  cha “Muungano Vijana Kilolo”kilichopewa msaada wa mashine na NHC ambapo walikagua kazi za vijana hao (hawapo pichani) ambapo Wilaya hiyo imeamua kuwapa mkopo vijana hao ili wawe na benki kubwa ya matofali.
New Picture (11)
Kikundi cha vijana cha “Umoja wa Wafyatua matofali” kilichopo katika Kata ya Mkwawa Manispaa ya Iringa kikiwa kimeanza kazi ya kutengeneza matofali kilipotembelewa na timu ya NHC kuona kazi zao. Hiki ni kikundi kinachofanya vizuri katika Manispaa hiyo yenye vikundi vinne vya vijana waliopewa msaada wa mashine na NHC za kufyatulia matofali ya kufungamana.. UMOJA WA WAFYATULA MATOFALI MANISPAA YA IRINGA
New Picture
Kikundi cha SHIDEPHA ambacho kilipewa mafunzo ya namna  ya kutumia mashine za kutengeneza matofali ya kufungamana  na NHC kikiwa imara na timu ya NHC iliyowatembelea  na kuamua kuwaongezewa uwezo kwa kupewa mafunzo na vifaa vya kufanyia kazi. Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC baada ya kuona juhudi zao aliamuru waongezewe mashine mbili ili wasonge mbele na Halmashauri imekitambua kikundi hicho.

No comments:

Rais wa Sierra Leone Awasili nchini

Rais wa Jamhuri ya Sierra Leone, Mheshimiwa Julius Maada Bio, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kilele wa Wak...