Friday, July 03, 2015

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LANG'ARA MAONYESHO YA 39 YA SABASABA

Afisa Mwandamizi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Salvatory Hinju akitoa maelezo namna Shirika la Nyumba linavyofanya kazi zake kwa Wateja waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika hilo lililopo ndani ya viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa, Tuntufye Mwambusi akizungumza na mmoja wa wateja wa Shirika la Nyumba alipofika kwenye banda la maonyesho la Shirika hilo lililopo ndani ya viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa.
 Mteja akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Aika Swai, anayewasikiliza ni Afisa Mauzo Mwandamizi wa NHC, Julieth Buberwa.
 Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Aika Swai akitoa maelekezo kwa wateja kuhusiana na ujenzi na mauzo ya nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba.
Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Chediel Msuya akitoa maelekezo kwa wateja kuhusiana na ujenzi na mauzo ya nyumba za gharama nafuu za Shirika la Nyumba la Taifa kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba.
 Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Vincent Ngaile akitoa maelekezo kwa mteja kuhusiana na ujenzi na mauzo ya nyumba za gharama nafuu za Shirika la Nyumba la Taifa kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba.
Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda akiingia kwenye viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba.
 Waziri Mkuu, Mizengo Kayanza Peter Pinda akiingia kwenye viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba.
Ujumbe kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara ya Afrika Kusini, ukimsikiliza Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Vincent Ngaile aliyekuwa akizungumza nao kuhusu shughuli mbalimbali za Shirika. Wanaomsikiliza ni Mkurugenzi wa Mkuu wa Ukuzaji Biashara na Masoko wa Idara ya Masoko na Mauzo ya Wizara hiyo, Zanele Sani.
Meneja Miradi Msaidizi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Hassan Mohammed akitoa maelekezo kwa mteja kuhusiana na namna matofali ya Hydraform yanavyotumika kujenga nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba.
Banda la Maonyesho la Shirka la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo langoni kuu la kuingilia kushoto kama unaingia Viwanja vya Mwalimu Nyerere kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea.
Ujumbe kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara ya Afrika Kusini, uukizungumza na maafisa wa  Shirika la Nyumba la Taifa  kuhusu shughuli mbalimbali za Shirika. Wanaomsikiliza ni Mkurugenzi wa Mkuu wa Ukuzaji Biashara na Masoko wa Idara ya Masoko na Mauzo ya Wizara hiyo (mwenye miwani), Zanele Sani.
Mkuu wa Ukuzaji Biashara na Masoko wa Idara ya Masoko na Mauzo ya Wizara hiyo, Zanele Sani  (mwenye miwani) na Ujumbe kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara ya Afrika Kusini, wakizungumza na maafisa wa Shirika la Nyumba la Taifa kuhusu shughuli mbalimbali za Shirika. 
Afisa Kituo cha Huduma kwa Wateja cha NHC, Theresia Muhondo akitoa maelekezo kwa wateja kuhusiana na ujenzi na mauzo ya nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...