Mafundi wa kampuni ya kuhifadhi mafuta ya Tanzania International Petroleum Reserves Limited (TIPER), wakitengeneza paa katika moja ya matanki mapya ya kampuni hiyo, wakati kampuni hiyo ikitaraji kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta maradufu baada ya kukamirika kwa ukarabati wa matanki yake wawili ya mita za ujazo 36,600 kila moja ifikapo machi mwaka huu.
Miongoni mwa matanki ya kampuni ya ya kuhifadhi mafuta ya Tanzania International Petroleum Reserves Limited (TIPER) yanayofanyiwa marekebisho, wakati kampuni hiyo ikitaraji kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta maradufu baada ya kukamirika kwa ukarabati wa matanki yake wawili ya mita za ujazo 36,600 kila moja ifikapo machi mwaka huu
Kampuni ya kuhifadhi mafuta ya Tanzania International Petroleum Reserves Limited (TIPER) inatarajia kuongeza uwezo wake wa kuhifadhi mafuta mara mbili zaidi baada ya kukamilika kwa ukarabati wa matanki yake mawili, yenye mita za ujazo 36,600 kila moja, ifikapo mwezi Machi mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo jana, mradi huo uliozinduliwa mapema mwaka jana, unawakilisha uwekezaji wa Dola za kimarekani milioni 11 (Takribani 19bn/-) na utapelekea kuongezeka kwa uwezo wa kuhifadhi mafuta kutoka mita za ujazo 141,000 na kufikia mita za ujazo 213,200 mara baada ya kukamilika.
“Zaidi ya hayo, muundo mpya wa muunganiko wa bomba utaongeza ufanisi wa kupokea mafuta ya ‘Automotive Gas Oil’ (AGO) kutoka kwenye ‘Single Point Mooring’ (SPM) kutoka kwenye kiwango cha mtiririko ‘flow rate’ cha mita za ujazo 1,500 kwa saa mpaka kufikia mita za ujazo 2,000 kwa saa, ambacho ni kiwango cha kasi zaidi,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa TIPER, Bw. Daniel Belair.
Ili kukidhi ukuaji wa mahitaji ya bidhaa ya mafuta, Bw. Daniel Belair alisema kuwa kampuni hiyo ina mpango wa kutengeneza matanki mapya ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi mafuta kwa mita za ujazo 100,000 zaidi ili kufikia mita za ujazo 313,200 katika siku zijazo.
Kufuatia mradi huo, Bw. Belair alisema kuwa TIPER ina mpango wa kutandaza mabomba mapya ya kusafirisha mafuta kati ya Kigamboni na Kurasini.
“Mradi huu utaongeza ufanisi wa kusukuma kwa kasi zaidi bidhaa kwa wateja wetu waliopo Kurasini,” alisema huku akiongeza kuwa uwekezaji huo utagharimu kati ya Dola za kimarekani milioni 12 na 16.
Wakati huohuo kampuni itawekeza kiasi kingine cha Dola za kimarekani milioni 2 ili kubadilisha mfumo uliopo wa kupampu kwa kuweka pampu zenye uwezo mkubwa zaidi na wenye kuaminika na pia mita za utiririkaji ‘flow meters’ zitaongezwa.
Kupitia taarifa hiyo, Bw. Blair aliweka bayana mpango wa kampuni hiyo wa kutenga kiasi cha dola za kimarekani milioni 2 zitakazotumika kufanyia marekebisho mpango wake wa kukabiliana na dharura ‘Emergency Response Plan’ ili kwenda sambamba na uwezo huo mpya. Alisema kuwa kitengo cha kupambana na janga la moto pia kitaimarishwa zaidi.

No comments:
Post a Comment