Thursday, February 12, 2015

EFM YAANDAA HAFLA YA VALENTINE

………………………………………………..
Kila mwaka,tarehe 14 Februari,watu duniani kote huadhimisha siku ya wapendanao duniani.
Kama ilivyo ada,wengi wetu tumezoea kuadhimisha siku hiyo na aidha mume,mke au mpenzi.
Ila kituo cha redio cha 93.7 EFM, kinawapa nafasi ya kipekee wasikilizaji wao kuchagua mtu ambaye wao ndio wanamuona kama mchizi wao.
Meneja Uhusiano wa 93.7 EFM,Kanky Mwaigomole,amesema mchizi wako sio lazima awe mpenzi wako,bali anaweza kuwa kaka,dada,jirani,bosi wako au hata mama mkwe wako,wote hao wanaweza kuwa mchizi wako.
“Sio lazima kila mwaka tufanye mambo yale yale,tumeona tufanye mabadiliko kidogo,alisemea meneja huyo.
Siku ya “wewe ndio mchizi wangu”,itafanyika pale Msasani Beach Club,siku ya tarehe 14 mwezi huu wa February mwaka 2015,ambapo itahusisha wasanii kama vile Mesen Selecta (Mzee wa kanya boya),Recho Kizunguzungu,Msaga sumu,Snura, Sir Juma Nature,RDJ Majay akiwa na Zungu the drama na wengine kibao.
Kanky alisema kwamba ukija na mchizi wako,kutakuwa na zawadi kubwa sana kutoka kwa DJ Majay na Zungu the drama.
“Tunaomba watanzania wajitokeze kwa wingi,kwani watangazaji wote watakuja kupiga picha na kuongea na mchizi wa EFM 93.7.Bado tunaendelea kuwaleta wasikilizaji wetu karibu na sisi,kama mnakumbuka mwaka jana,tuliwaletea tamasha la “Mziki Mnene”,ambapo tulipata nasafi kubwa ya kujumuika na washabiki wetu kwa mda wa miezi mitatu mfululizo,na tukawaahidi kuwaletea mambo mengi mbele ya macho yao”,alisema meneja uhusiano huyo.
Kanky alisema kuwa,zawadi nyingi zitatolewa kwa mtu na mchizi wake na pia kutakua na michezo mbali mbali ambayo itafanyika siku hiyo ya 14 February 2015.
Aliendelea na kusema kwamba hii sio tamasha bali watu waje na machizi wao kuja kuchizika,ni kuanzia saa kumi jioni mpaka watakapo choka.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...