Friday, February 13, 2015

VIJANA CUF KUANDAMANA LEO PAMOJA NA KUONYWA NA POLISI

 Mwenyekiti
wa Jumuia ya Vijana wa CUF Taifa (JUVICUF), Hamidu Bobali akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Februari 12,2015 kuhusian na
maandamano yatakayo fanyika kesho licha ya kukosa kibali cha Jeshi la
Polisi. Pamoja nae ni Mjumbe wa jumuia hiyo, Shani Beleko. Kwa hisani ya http://mrokim.blogspot.com/
 Wanahabari wakichukua dondoo za mkutano huo.
Baadhi ya vijana ambao ni wanachama wa JUVICUF wakiwa katika mkutano huo.
************
CHAMA cha
Wananchi  CUF kupitia Jumuiya ya Vijana
wa Chama cha Wananchi (JUVICUF), kime[panga kufanya maandamano makubwa leo Februari
13, 2015 kuanzia Bugururuni Rosana hadi Ofisi za Tume ya taifa ya Uchaguzi na
baade Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kwa mujibu
wa Mwenyekiti wa JUVICUF, Hamidu Bobali amesema maandamano hayo yamenyimwa
kibali na jeshi la Polisi lakini kwakuwa walisha jiandaa kuyafanya wao
watayafanya ili kufikisha ujumbe wao .
“Tumeandaa
manaandamano ya amani  kwa lengo la  kuitaka tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC),kuongeza
siku za kuandikisha wapiga kura kutoka saba (7) zilizo pangwa sasa hadi 14 na
kulaani  ukiukwaji wa haki za binadamu
unaofanywa na polisi,” alisema Bobali.
Bobali Februari
9,mwaka huu waliliandikia jeshi la polisi barua ya  kuwataarifu juu ya kufanyika kwa maandamano
hayo ya amani  na waliainisha maudhui ya
maandamano hayo na kuwa ni kuitaka NEC,kuongeza siku za kuandikisha wapiga kura
kutoka siku saba hadi 14, na kulaani ukiukwaji wa haki za binadamu  waliodai unafanywa na  jeshi hilo.
Majibu ya
barua hiyo yaliyotolewa jana na jeshi
hilo, yamesitisha maandamano hayo kwa madai kuwa njia hiyo haiwezi kuleta
suluhu la madai yao.
Maandamano
hayo yamepamngwa kuanzia saa nne asubuhi.
Kufuatia sakata hilo, Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Suleiman Kova akizungumza na vyombo vya habari ofisi kwake ametangaza kupiga
marufuku maandamano hayo kwa kile alichoeleza kuwa yana leongo la kuvunja
amani.
Kamishna Kova amesema Jeshi la Polisi watatumia
uwezo wao kwa misingi ya sheria ili kudhibiti maandamano hayo ambayo hayana nia
nzuri. 
“Maandamano yao hayana mantiki yoyote, tuliwaita
viongozi wao ambao ni Maulid Said Naibu Katibu na Masoud Said Masoud ili
waongozane na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu  kwenda NEC kupata ufumbuzi wa maoni yao,”
alisema Kova.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...