Tuesday, February 17, 2015

Watanzania waendelea kunufaika na gharama nafuu za mawasiliano


Mkurugenzi Mtendaji waVodacom Tanzania Rene Meza, akiongea na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini hotuba aliyokuwa akitoa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (hayupo pichani) juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia akijibu waswali ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Rene Meza kuongelea juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni jijini Dar es Salaam jana. 

Watanzania wanaotumia huduma za mawasiliano  bado wanaendelea kupata huduma hizo kwa gharama nafuu kwa kupiga simu na  matumizi ya interneti ukilinganisha na huduma zinazotozwa kupata mawasiliano katika nchi nyingine za Afrika ikiwemo Afrika ya Kusini,Kenya,Nigeria na  hata nchi ya india.

Haya yaemebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza,katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo alitoa mfano kuwa licha ya ongezeko la bei katika vifurushi vya kupata huduma mawasiliano bado katika kifurushi cha gharama ya chini ambayo ni shilingi 500 mteja anaweza kupata MB za kutosha kutumia internet ikiwemo kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS).

Alitoa mfano kuwa mteja akinunua kifurushi cha shilingi 500,kati ya hizo fedha shilingi 138  inakwenda serikalini kwa ajili ya kodi na kampuni kubakia na shilingi 362/- ambapo fedha hizo zinamuwezesha kupata muda wa dakika 15 za maongezi ikiwa kila dakika inatozwa shilingi 24/-,MB za kuperuzi internet  8 kila MB ikiwa inatozwa shilingi 5 na kutuma ujumbe wa maneno (SMS) 250 ambapo kila ujumbe natozwa shilingi 0.12

“Viwango vya malipo  kwa Vodacom ni vya gharama nafuu na vimepangwa kulingana na mahitaji ya wateja wetu licha ya mabadiliko  madogo katika bei yaliyofanywa hivi karibuni.Hivi sasa tunatoza shilingi 4.9/-kwa kila MB katika kifurushi cha GB5 ambapo bei ya awali kilikuwa kinatozwa shilingi 3.9/-.Bado malipo ya sasa ni madogo ukilinganisha na mallipo yanayotozwa kwenye kifurushi cha GB5  kwenye soko la  huduma za mawasiliano  kwa fedha za kitanzania kwa mfano Nigeria  inatoza shilingi 17/-/Afrika ya Kusini Shilingi 13/-,Kenya shilingi 12/-,Ghana shilingi 7/-na India shilingi 5/-

Meza pia alielezea mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na kampuni ya Vodacom katika kipindi cha mwaka 2014 amabpo aliwashukuru wateja wote kuwa wamechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa mafanikio hayo ikiwemo zaidi ya wateja 1.7 kujiunga na familia ya Vodacom.

Pia alisema kuna ongezeko la wateja wanaoendelea kufaidika na huduma mbalimbali zinazotolewa na Vodacom ikiwemo huduma ya internet ya gharama nafuu na huduma nyinginezo kama vile M-Pesa ambayo imekuwa na mafanikio kwa kuwa na mtandao wa mawakala 85,000 na  kufanya mihamala inayofikia Trioni 1.2  kwa mwaka  pia huduma ya M-Pawa imekuwa kwa kasi na inawawezesha wateja wengi kuweka pesa na kukopa.Pia aliongeza kuwa kampuni imeongoza kwa  kuwa ya pili kulipa na kukusanya kodi za serikali  na kuwa ya kwanza katika sekta ya mawasiliano.

Alisema kwa mwaka  jana kampuni iliweza kuwekeza shilingi bilioni 180/- na mwaka huu itawekeza shilingi bilioni 140/- katika kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya internet na kusambaza huduma bora kwa wateja nchini kote.

Alimalizia kwa kusema kuwa moja ya dhamira ya kampuni ni kuunga mkono juhudi za kusambaza huduma nchini kote hususani sehemu za vijijini ambapo katika kuunga mkono jitihada hizi kampuni imekuwa ikichangia fedha kwenye mfuko wa kusambaza huduma za mawasiliano vijijini ujulikanao kama UCAF.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...