Thursday, February 26, 2015

CHID BENZ: ATOZWA FAINI, AAHIDI KUACHA MADAWA YA KULEVYA

Chid Benz (mwenye shati jeupe) baada ya kuachiwa na mahakama.
…Akiondoka mahakamani.…
…Akielekea kwenye gari lililomleta.
MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Rashidi Makwilo maarufu kama ‘Chid Benz’,  aliyekuwa anatuhumiwa kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin  na bangi, leo ameachiliwa huru kwa kulipa faini ya Sh. 900,000.
Katika maelezo ya awali yaliyosomwa na mwendesha mashtaki wa Jamhuri Diana Lukendo, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, msanii huyo  alimwambia hakimu  kuwa mshtakiwa alikamatwa na dawa hizo za kulevya akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl.  Julius  Nyerere,  akitaka kusafiri kuelekea mkoani Mbeya.
Hata hivyo mshtakiwa huyo ambaye alikiri kosa  mnamo tarehe 18 Aprili mwaka huu, leo aliiomba mahakama kumpunguzia  adhabu  na kwamba asingetumia tena ulevi huo na atawaelimisha vijana wenzake juu ya madhara yake.
(NA GABRIEL NG’OSHA NA LAURENT SAMATTA/GPL)

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...