Wednesday, February 25, 2015

VURUGU KUBWA IRINGA, POLISI NA WANANCHI WAPAMBANA.

 
Zipo taarifa za kutokea kwa vurugu kubwa katika eneo la Ilula mkoani Iringa.Taarifa zinadai kuwa vurugu hizo ni kati ya jeshi la polisi na wananchi wa kawaida ambao wamefunga barabara kwa kuwasha moto wa matairi ya gari.
Aidha taarifa kutoka kwenye eneo la tukio zinaendelea kueleza kuwa hadi sasa magari manne ya Polisi na Pikipiki moja vimechomwa moto, huku basi linalofahamika kwa jina la Nyagawa linalosafirisha abiria kutoka Njombe kwenda Dar es Salaam likiwa limevunjwa vioo vyote.
Taarifa hizo zinadai kuwa tayari polisi wa kutuliza ghasia FFU wameshafika eneo la tukio na kufanikiwa kwa sehemu kutuliza ghasia hizo, na kwamba magari yanayokuja Dar es Salaam na mikoa mingine yameshaanza safari zake.
Ungana nasi baadaye kwa taarifa zaidi
Chanzo Mwananchi
 …………………………………
PICHA KWA HISANI YA IRINGA YETU BLOG

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...