Friday, February 13, 2015

WAZIRI CHIKAWE AZINDUA MNARA WA TTCL NACHINGWEA

ch1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya TTCL katika Kata ya Kiegei, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika katika Kijiji cha Kiegei jana, ambapo viongozi wa Mkoa, Wilaya pamoja na mamia ya wananchi kutoka vijiji vilivyonufaika na mtandao huo wa mawasiliano vya Kiegei A, B, Namatunu, Nanjihi, Kilimarondo, Mbondo, Nahimba na Nakalonji walihudhuria shehere hizo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
ch2Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akipiga simu ya Kampuni ya  na Nicodemus Mngulu Meneja wa Kampuni hiyo mkoani Lindi kulia baada ya kuzindua rasmi mnara mkubwa wa mawasiliano wa Kampuni hiyo katika Kata ya Kiegei, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika katika Kijiji cha Kiegei jana, ambapo Viongozi wa Mkoa, Wilaya pamoja na mamia ya wananchi kutoka vijiji vilivyonufaika na mtandao huo wa mawasiliano vya Kiegei A, B, Namatunu, Nanjihi, Kilimarondo, Mbondo, Nahimba na Nakalonji walihudhuria shehere hizo. Aliyevaa kofia (kulia) ni Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya TTCL, Kanda ya Zanzibar, Hussein Nguvu. Picha na Felix Mwagara.
ch3Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kulia) akimuuliza swali Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Simu ya TTCL, Kanda ya Zanzibar, Hussein Nguvu (wapili kushoto), baada ya kuuzindua mnara wa mawasiliano wa Kampuni hiyo katika Kata ya Kiegei, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika katika Kijiji cha Kiegei jana, ambapo viongozi wa Mkoa huo, Wilaya pamoja na mamia ya wananchi kutoka vijiji nane vilivyonufaika na mtandao huo wa mawasiliano walihudhuria shehere hizo. Wapili kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo, na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Lindi, Revetha Mzinga.Picha na Felix Mwagara.
ch4Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na mamia ya wananchi (hawapo pichani) kabla ya kuuzindua mnara wa Kampuni ya Simu ya TTCL katika Kata ya Kiegei, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Katika hotuba yake, Chikawe aliwataka wananchi zaidi ya 1200 ambao mpaka sasa tayari wameunganishwa na mtandao huo, kutumia vizuri simu zao za mkononi kwa kutokujiingiza katika uhalifu wa aina yoyote, kwani endapo watafanya hivyo Jeshi la Polisi litawakamata. Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika katika Kijiji cha Kiegei jana. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo, kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Lindi, Revetha Mzinga na kulia ni Mkuu wa Biashara wa Kampuni hiyo, Kanda ya Zanzibar, Hussein Nguvu. Picha na Felix Mwagara.
ch5Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akipokea zawadi ya simu ya mezani kutoka kwa Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Simu ya TTCL, Kanda ya Zanzibar, Hussein Nguvu baada ya Waziri huyo kuuzindua mnara wa Kampuni hiyo katika Kata ya Kiegei, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Katika hotuba yake, Chikawe aliwataka wananchi zaidi ya 1200 ambao mpaka sasa tayari wameunganishwa na mtandao huo, kutumia vizuri simu zao za mkononi kwa kutokujiingiza katika uhalifu wa aina yoyote, kwani endapo watafanya hivyo Jeshi la Polisi litawakamata. Sherehe za uzinduzi huo zilifanyika katika Kijiji cha Kiegei jana. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...