Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiongea na viongozi wa CCM wa Tawi la Ufukoni katika Kata ya Rahaleo huko Lindi Mjini tarehe 9.2.2015. Mama Salma Kikwete yupo wilayani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku 5.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Lindi Mjini Dkt. Zulfa Msami wakati Mama alipotembelea kituo hicho tarehe 10.2.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwangalia mtoto mwenye umri wa siku 2 aliyeshikwa na Mama yake Sharifa Ali,19, wakiati Mama Salma alipotembelea kituo cha Afya cha Lindi Mjini tarehe 10.2.2015.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa anayewakilisha Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akiwa amempakata mtoto Adaita Hamis mwenye umri wa siku 1 aliyezaliwa katika Kituo cha Afya cha Lindi Mjini tarehe 9.2.2015 huku akiongea na mama wa mtoto huyo Bibi Zanida Ismail,42, anayeishi Mtaa wa Benki huko Lindi Mjini wakati Mama Salma alitembelea kituoni hapo tarehe 10.2.2015.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment