Tuesday, February 17, 2015

Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta Amsimamisha Kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Eng Madeni Shamte Kipande

 Picha Juu ni Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samuel Sitta akizungumza na wanahabari leo bandarini) amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Eng Madeni Shamte Kipande kwa tuhuma za utendaji mbovu, ikiwa ni pamoja na kutokuwepo kwa uwazi kwenye mamlaka hiyo hususani katika michakato ya zabuni mbalimbali zinazotangazwa na mamlaka hiyo.

Pamoja na kuchukua uamuzi huo Mhe. Sitta, ameunda tume ya watu sita itakayokuwa na jukumu la kuchunguza tuhuma zinazomkabilia Mhandisi Kipande ambaye atakuwa nje ya madaraka kwa muda wa wiki mbili kupisha uchunguzi huo na nafasi yake itakaimiwa na Meneja wa Bandari Dar es Salaam Bw. Awadhi Masawe.
 

 
Kipande aliteuliwa kushika wadhifa huo mnamo mwaka 2012 mwezi Agosti na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe. Picha Zote na Francis Dande 

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...