Friday, February 27, 2015

KIPINDI CHA “JICHO LETU MKURANGA” CHA REDIO UPENDO CHASAIDIA JAMII YA WENYE MAHITAJI MUHIMU MKURANGA

DSC_2663Mchungaji Chedie Lwiza ambaye ni msaidizi wa Dr. Alex Malasusa Askofu mkuu wa Kanisa la KKKTDayosisi ya Mashariki na Pwani akikabidhi madawati kwa Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Bw.Benjamin Majoye yaliyotolewa na Benki ya Maendeleo na Kampuni ya FIFA Flow Traiding Company Limited ya jijini Dar es salaam pamoja na vifaa mbalimbali zikiwemo sare za shule, madaftari na viatu kutokana na msaada mkubwa wa kipindi cha “Jicho letu Mkuranga” kinachorushwa kila siku na kituo cha Redio cha Upendo Media cha jijini Dar es salaam kwa kuibua changamoto hizo na kuhamasisha taasisi na wananchi mbalimbali wenye uwezo kusaidia jamii masikini na zenye mahitaji muhimu, katika picha wa pili kutoka kulia ni Frank Mbando Mkurugenzi wa Kampuni ya FIFA Flow na katikati ni Ibrahim Mwangalaba Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo PLCDSC_2664Mchungaji Chedie Lwiza ambaye ni msaidizi wa Dr. Alex Malasusa Askofu mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Kanisa la KKKT akikabidhi sare za shule  kwa Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Bw.Benjamin Majoye zililzotolewa na Benki ya Maendeleo na Kampuni ya FIFA Flow Traiding Company Limited ya jijini Dar es salaamDSC_2667Ibrahim Mwangalaba Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo PLC akitoa shukurani zake kwa wageni mbalimbali mara baada ya kukabidhi madawati na vifaa mbalimbali vya shule kwa mkuu wa wilaya ya Mkuranga.DSC_2642Nang’ida Johanes Lairumbe Mkurugenzi wa Upendo Media akitoa utambulisho kwa viongozi mbalimbali waliofika katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika jengo la Luther House jijini Dar es salaam, Kutoka kulia ni Frank Mbando Mkurugenzi wa Kampuni ya FIFA FlowTraidinga, Mchungaji Chedie Lwiza ambaye ni msaidizi wa Dr. Alex Malasusa Askofu mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani na Ibrahim Mwangalaba Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo .DSC_2652Mchungaji Chedie Lwiza ambaye ni msaidizi wa Dr. Alex Malasusa Askofu mkuu wa Kanisa la KKKTDayosisi ya Mashariki na Pwani akitoa shukurani zake kwa Benki ya Maendeleo na Kampuni ya FIFA Flow Traiding kwa msaada wa madawati na vifaa mbalimbali vya shule walivyovitoa kwa wilaya ya Mkuranga.DSC_2658Picha ya pamoja viongozi hao wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyokabidhiwa kwa wilaya ya Mkuranga.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...