Thursday, February 19, 2015

MAMA SALMA KIKWETE ATILIANA SAINI MKATABA WA UPANUZI WA SHULE YA WAMA-NAKAYAMA NA BALOZI WA JAPAN HAPA NCHINI MHE. MASAKI OKADA.

1
Balozi wa Japan nchini Tanzania Mheshimiwa Masaki Okada akizumgumza na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete pamoja na uongozi wa Taasisi hiyo muda mfupi kabla ya kutiliana saini mkataba wa mradi wa kupanua Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama iliyoko Rufiji, Mkoani Pwani tarehe 19.2.2015.
2
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akitiliana saini na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaki Okada kwenye mradi wa upanuzi wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama utakaogharimu dola za kimarekani 498,738. Sherehe ya utiaji saini ilifanyika kwenye ofisi za WAMA zilizopo karibu na Ikulu.
4
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akibadilishana hati za Mkataba na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaki Okada mara baada ya kutia saini zao kwenye mkataba huo.
5
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akizungumza mara baada ya kumaliza kutiliana saini mkataba wa mradi wa upanuzi wa Shule ya WAMA Nakayama.
6
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan hapa nchini Mheshimiwa Masaki Okada mara baada ya viongozi hao kutia saini mkataba wa upanuzi wa Shule ya Sekondari WAMA-Nakayama.
PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...