Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) akimkaribisha Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kushoto) ili aweze kuzungumza na timu ya majaji na sekretarieti iliyofanya kazi ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Utoaji wa Huduma za Jamii na Uwezeshaji kwa makampuni ya uziduaji yaani madini na gesi. Timu hiyo iliendesha zoezi hilo mapema Septemba, mwaka jana.
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kushoto) akisisitiza jambo katika kikao hicho. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi MwihavaWaziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene akielezea umuhimu wa kuhamasisha makampuni mengi zaidi kujitokeza katika kuwania tuzo ya Rais katika utoaji wa huduma kwa jamii na uwezeshaji kwa makampuni ya gesi, mafuta na madini ili wananchi wafaidike zaidi na mchango katika sekta za nishati, madini na gesi.
No comments:
Post a Comment