Christian Bella (kulia) akijibu baadhi ya maswali ya wanahabari (hawapo pichani) kuhusu maandalizi ya shoo yake ya Valentine kwenye Ukumbi wa Dar Live.
Bella akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani).
Christian Bella (kulia) akiwapa vionjo vya wimbo wake mpya wa ‘NASHINDWA’ wanahabari (hawapo pichani). Kushoto ni mmoja wa viongozi wa Malaika Band, X-Bass Babu Bomba.
Bella akitoa vionjo vya wimbo wa ‘NANI KAMA MAMA’ kwa wanahabari.
Bella akiwa na Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist.
X-Bass Babu Bomba na Bella katika pozi na Mpiga Picha wa GPL, Musa Mateja.
X-Bass Babu Bomba na Bella wakiwa katika picha ya pamoja na Mhariri Mwandamizi wa GPL, Walusanga Ndaki.
X-Bass Babu Bomba na Bella wakipozi na Shafii Mohamed wa GPL.
X-Bass Babu Bomba na Christian Bella katika pozi ndani ya GPL.
PREZIDAA wa Bendi ya Malaika Music, Christian Bella ‘King of the Best Melodies’ amewaahidi shoo kali mashabiki wake watakaohudhuria katika Ukumbi wa Kisasa wa Dar Live, Jumamosi ijayo ambayo ni Siku ya Wapendanao ‘Valentine’s Day’.
Staa huyo ameyasema hayo hivi punde wakati wa mkutano na wanahabari wa vyombo mbalimbali uliofanyika katika ofisi za Global Publishers.
Bella amesema atakuwepo ndani ya kiwanja hicho mapema kuanzia saa 7 mchana na atapiga picha za red carpet na mashabiki wake watakaohudhuria sambamba na kuzungumza nao mawili-matatu.
Mbali na kuwahi ukumbini, Bella amewaandalia nyimbo zake zote kali za mapenzi kama vile Msaliti, Safari Siyo Kifo, Nakuhitaji pamoja na wimbo bora uliofunga mwaka wa Nani Kama Mama.
Kuonyesha kuwa utakuwa Usiku wa Wapendanao, Bella amewaandalia mashabiki wake zawadi ya wimbo mpya uitwao NASHINDWA ambao atauchia kwa mara ya kwanza huku video akienda kuifanyia nchini Afrika Kusini wiki ijayo.
Mbali na Bella usiku huo ambao ni maalum kwa wapendanao, mkali wa muziki wa Mwambao, Mfalme Mzee Yusuf naye atakuwepo katika kuwaburudisha mashabiki wote watakaokuwepo ukumbini hapo.
Usiku huo Mzee Yusuf atashuka na kundi lake la Jahazi Modern Taarab na kuangusha ngoma zake zote kali za mapenzi kama vile My Valentine, Wapendanao, Tiba ya Mapenzi, Wasiwasi Wako pamoja na hii ambayo ni habari ya mjini kwa sasa ya Mahaba Niue.
No comments:
Post a Comment