Friday, February 20, 2015

TIGO KUWEKEZA DOLA ZA KIMAREKANI 120 KUTANUA MTANDAO WAKE 2015

tigo1
Kaimu Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania Cecile Tiano akiongea na waandishi wa habari kuhusu kampuni yake itakavyowekeza mwaka huu, pembeni yake Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha.
Sent from Huawei Mobile
……………………………………………………………………………….
Tigo Tanzania imepanga kutumia kiasi cha dola milioni 120 (Shilingi bilioni 221) mwaka huu kwa ajili ya upanuzi wa mtandao wake utakao ongeza ufanisi wa huduma zake nchini.
Akizungumza mipango hiyo ya kampuni kwa mwaka 2015, Kaimu Meneja Mkuu wa Tigo Bi.Cecile Tiano alisema kwamba uwekezaji wa mwaka huu ni ishara ya nyongeza ya asilimia 20 kutoka dola milioni 100 za kimarekani (shilingi bilioni 184) ambazo kampuni ilitumia katika kuboresha ufanisi wake kwa mwaka 2014. 
“Ongezeko hili la uwekezaji inadhihirisha nia yetu ya dhati katika kuwapatia wateja wetu huduma bora ambazo zinapitiliza matarajio yao na kuwapa Watanzania wengi zaidi uwezo wa kupata huduma ya mawasiliano nchini,” alisema Tiano. 
Akielezea mwaka 2014 kama msimu mzuri, Meneja Mkuu huyo alisema kwamba Tigo imeweka rekodi ya kukua kwa idadi yao ya wateja kutoka milioni saba na kufika milioni 9 ambayo ni sawa na asilimia 30.
“Tunataka kupanua na kuendeleza ubora wa mtandao wetu kwa kuwekeza katika minara 787 nchini kote. Baadhi ya minara hii yatakua yana uwezo wa intanet mwendo kasi 4G na zingine 3G, ambayo ina maanisha kwamba maeneo ya vijijini yatazidi kufikiwa zaidi pamoha na uwezo wa wateja wetu kutumia zaidi vifurushi vya data,” alisema huku akitaja kwamba Tigo ina minara zaidi ya 2,000 nchini kote. 
Mipango mengine kwa ajili ya 2015, kutokana na maelezo ya Tiano, ni ongezeko la mara mbili ya idadi ya matawi ya huduma kwa wateja za Tigo kutoka 42 zilizopo sasa hadi 100 kwa ajili ya kuleta huduma za Tigo karibu zaidi na wateja. 
Ili kuweza kuendeleza mabadiliko ya kidijitali nchini, Meneja huyo alisema kwamba Tigo ina mpango wa kuzindua bidhaa na huduma zingine za kibunifu mwaka huu kama ambavyo huduma ya ‘Tigo Music’ iliyozinduliwa hivi karibuni imeweza kubadilisha tasnia nzima ya mziki kwa kuwapatia wateja wa Tigo muziki ya kitaifa na kimataifa kupitia simu zao za mkononi. 
Hii huduma ya kipekee ilitanguliwa na huduma zingine nyingi ambazo Tigo ilikuwa kampuni ya kwanza ya simu kuzindua mwaka jana ikiwemo huduma ya kutuma na kupokea fedha ya kimataifa yenye uwezo wa kubadilisha aina ya Ankara moja kwa moja kwenye simu, huduma ingine ni Facebook ya Bure kwa lugha ya Kiswahili. Tigo ndani ya mwaka 2014 pia iliunganisha huduma zake za kutuma na kupokea fedha na benki kubwa zinazoongoza nchini ili kuwawezesha wateja kuweka na kutoa fedha kutoka katika akaunti zao za benki kupitia akaunti za simu za Tigo Pesa. Muundo wa aina hiyo wa ushirikiano pia ulianzishwa na Tigo Pesa ili kuweza kutuma na kupokea fedha kwa namna rahisi zaidi kwenda mitandao mingine. 
Aliongeza kwamba Tigo itaendelea kutoa msaada mbali mbali ya maendeleo kwa jamii kupitia mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii ya mwaka 2015 ambayo itajumuisha sekta ya elimu, afya, huduma za wanawake na watoto.

No comments: