Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya wawekezaji wa sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI) Bi. Pamela Mattheuu (aliesimama) akielezea hali ya Utalii ilivyo kwa sasa na kupanga mikakati ya kuitangaza zaidi sekta hiyo, huko Hoteli ya Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya wawekezaji wa sekta ya Utalii Zanzibar Nd. Abdulsamad Said akizungumza na wanachama kuhusu mafanikio na changamoto zinazokabil sekta ya Utalii nchini katika Mkutano Mkuu uliofanyika Hoteli ya Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma (Mabodi) akifungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya wawekezaji wa sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI) katika Hoteli ya Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Baadhi ya wanachama wa Jumuiya hiyo wakimsikiliza mgeni rasmin Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma (Mabodi) kayupo pichani alipokuwa akifungua mkutano huo.
Mmoja wa wanachama wa ZATI Simai Mohamed Saidi akiuliza suali katika Mkutano huo uliofanyika Double Tree by Hilton Shangani Mjini Zanzibar.
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma (Mabodi) wakatikati katika picha ya pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa Jumuiya ya (ZATI) Abdulsamad Said (kulia) na kushoto Makamu wake mstaafu Boby Mckena. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
No comments:
Post a Comment