Friday, February 20, 2015

VIONGOZI WAUWAGA MWILI WA MAREHEMU SALMIN AWADH SALMIN BARAZA LA WAWAKILISHI

SIMA1Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Lowasa akiingia katika ukumbi wa baraza la wawakilishi kuuwaga mwili wa aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Marehemu Salmin Awadh Salmin aliefariki ghafla jana. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).SIMA2Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  kuuwaga mwili wa Marehemu Salimn Awadh.SIMA3Mwili wa Marehemu Salmin Awadh  ukiingizwa  katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani kwa ajili ya kuagwa rasmi.SIMA4Viongozi mbali mbali  wakijumuika na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakitoa heshma za mwisho kwa marehemu Salmin Awadh Salmin katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.SIMA5Viongozi mbali mbali akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Muhammed Shein wakimuonbea dua Marehemu Salmin Awadh baada ya sala iliyofanyika Masjid Noor Muhammad (SAW).SIMA6SIMA7Naibu Katibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai  na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mahmoud Muhammed wakibadilisha mawazo kuhusu msiba huo. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo ZanzibarSIMA8Mamia ya wananchi waliohudhuria sala ya kumuombea Marehemu Salmin Awadh Salmin wakiutoa msikitini mwili wa marehemu kuelekea kijijini kwao Makunduchi kwa mazishi.SIMA9Msafara uliobeba mwili wa Marehemu Salmin ukiondoka Masjid Noor Muhammad (SAW) kuelekea Makunduchi kwa ajili ya mazishi.
(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

No comments: