Thursday, February 19, 2015

WASANII WA FILAMU NCHINI WATAKIWA KUTOKUWA MAKONTENA YA BIASHARA HARAMU

 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo akizungumza na wasanii wa bongo movie wanaotarajia kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment iliyopo nchini Uingereza. Kulia ni Mama wa Didas Bi. Nuru Idrisa  
 Kutoka kulia Msanii Yusuph Mllela, Afisa kutoka Bodi ya Filamu Bibi Beatrice Msumari, Msanii Esha Buhet na Msanii Husna Athumani wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu walipofika ofisini kwake kwa ajili ya kuwaaga wasanii hao wanaotarajia kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment.
 Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo kulia akimpa mkono msanii Yusuph Mllela baada ya neno la kuwaaga wasanii watatu (Yusuph Mllela, Esha Buhet na Husna Athumani) wanaotarajia kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment.
 Msanii wa Bongo Movie Bi. Esha Buhet kushoto akifurahi wakati wa kuagana na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo kwa ajili ya kuanza safari ya kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na kampuni ya Didas Entertainment. Katikati ni Mama wa Didas Bi. Nuru Idrisa.
Msanii Husna Athumani akipokea mkono wa pongezi kutoka kwa Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo (kulia) wakati wa kuwaaga wasania wanaotarajia kwenda nchini Uingereza kurekodi filamu na Kampuni ya Didas Entertainment. Katikati ni Mama wa Didas Bi. Nuru Idrisa.          (Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo)         

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...