Friday, February 27, 2015

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MASHINE YA KUPIMIA SARATANI YA MATITI KWA AKINA MAMA HOSPITALI KUU YA JESHI LUGALO

mam10 
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akikabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwa uongozi kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kulia). Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye Hospitani Kuu ya Jeshi Lugalo kwenye Kitengo cha Uzazi na Mtoto kilichoko Mwenge tarehe 27.2.2015. Aliyesimama pembeni kwa Mama Salma ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando na aliyesimama kulia kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi ni Mkuu wa Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugal Brigedia Jenerali Josia Mwita Makere.mam9
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake muda mfupi kabla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ta matiti kwa akina mama kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo. Hafala hiyo ilifanyika kwenye Kitengo cha Uzazi na mtoto cha hospitali hiyo kilichoko eneo la Mwenge hapa Dar tarehe 27.2.2015
.mam4
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshauri Ndugu Peter Charles,28, baba mzazi wa binti Irene mwenye umri wa miezi 3 na mkazi wa Mikocheni kupunguza baadhi ya nguo alizomfunika mtoto wakati hali ya hewa ni ya joto. Mama Salma alimpongeza Ndugu Peter kwa kuambatana na mke wake kwenda kliniki.mam11 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Bibi Mariam Omar aliyemshika mtoto wake Jane Winston aliyekuwa akisubirim kupata huduma hospitalini hapo wakati Mama Salma alipotembelea sehemu mbalimbali za Kitengo cha Uzazi na Mtoto mara baada ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama tarehe 27.2.2015.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...