Wednesday, February 10, 2016

KILELE CHA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo kwa Wananchi katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar zilizofanyika katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,(kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman Chande,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha kitabu cha Sheria ya mwaka Zanzibar (ZANZIBAR YEARBOOKOF LAW) Volume 4 baada ya kukizindua rasmi leo katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja,(kulia)Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu,(kushoto) naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Ali Abdalla,Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohammed Othman Chande.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi katika sherehe za siku hii ya sheria.
Baadhi ya majaji waliohudhuria katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake leo kwa Wananchi katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.

Mwanasheria Mkuu zanzibar Said Hassan Saidi akitoa maelezo mafupi na kumkaribisha jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu wakati wa sherehe za kilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (kulia) na Jiji Mkuu Tanzania Mohammmed Chande Othman wakati alipowasili viwanja vya Victoria Garden katika sherehe za kilele cha siku ya sheria Zanzibar.
Kikundi cha sanaa na maigizo cha Blackroot walipotoa igizo lao leo katika sherehe zakilele cha siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika viwanja vya Victoria Garden Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ,{Picha na Ikulu.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...