Baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na marufiko katika eneo la mashamba ya mbunga lijulikalo kwa jina la Nyalu
Baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na marufiko katika eneo la mashamba ya mbunga lijulikalo kwa jina la Nyalu
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifyeka majani kwa ajili ya njia kuelea eneo lilikubwana mafuriko katika eneo la mashamba ya mbunga Nyalu.
Rubani wa ndege ya Jeshi la Polisi, Flora Focas akimwokoa mama mjamzito na kumuingiza katika chopa iliyompeleka Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye aliamuru chopa hiyo imchuke mama huyo ili kuokoa miasha yake.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitokea kwenye eneo la pori kwenye mashamba ya mpunga ya Nyalu kwa ajili ya kuangalia watu waliozingirwa na maji ili wawezekuokolewa . Alikuwa amembatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela.
Akina mama wenye watoto wadogo mtoto wa wiki moja na miezi miwili kuondoka katika eneo la marufiko katika mashamba ya Nyalu lililopo wilaya ya Iringa Mjini.(Picha na MAGRETH KINABO –MAELEZO)
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimwangalia mtoto aliyeugua ugonjwa wa kipindupidu katika kituo cha afya cha Mtakatifu Lucas (Kambi ya ugonjwa huo) kwenye eneo la Mboliboli kutokana na marufiko yaliyotokea katika kijiji cha Idodi, Iringa ambayo yalisomba nyumba na vyoo baada ya mto Ruaha kujaa maji kubadilisha mkondo wake.
Baadhi ya wagonjwa wakiendelea kunywa maji maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu baada ya kukumbwa na ugonjwa huo katika kambi maalum ya ugonjwa huo iliyopo katika kituo cha afya cha Mtakatifu Lucas.kwenye wilaya ya Iringa Mjini.
No comments:
Post a Comment