Wednesday, February 10, 2016

ASILIMIA 10 YA WATANZANIA WANAMILIKI UCHUMI WA NCHI’

uw1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua  Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
uw2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua  Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
uw4uw5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kaipata maelezo kutoka kwa Bi Fatuma Kango kuhusu Msimbomilia  au Barcode baada ya kufungua Mkutano wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 9, 216. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
uw7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafisi nchini, Reginald Mengi baada ya kufungua mkutano wa  Wadau wa Uwezeshaji Wananchi  Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
uw8
 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa VICOBA, Devota Likokola   (wapili kulia ) wakati alipotembelea banda la Benki ya Posta Tanzania katika Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi  alioufungua kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha walimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebuni na kuanza kutekeleza Sera ya Uwekezaji ili kufikia lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi. 
“Taarifa zilizopo zinaonyesha ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki uchumi wa nchi na sera hiyo ndiyo inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha kwamba wananchi wanapata fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujenga na kufaidika na uchumi wa mchi yao,” alisema.
Waziri Mkuu amesema maeneo yanayolengwa na sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya haraka na yanayogusa maisha ya wananchi hasa katika sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu, ujenzi, biashara, utalii, madini, viwanda na usafirishaji.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Alisema Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa nchi yetu inamilikiwa na Watanzania wenyewe. Waziri Mkuu pia alizindua Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu, Bibi Jenista Mhagama alisema hadi sasa mikoa 20 imekwishatenga maeneo ya uwekezaji kwenye halamhashauri zake  na imeanza kuweka miundombinu ya kuvutia wawekezaji.
Naye Mweyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Prof. Omari Issa alisema katika dunia ya sasa imebainika kuwa haina maana kumpatia mtu mkopo bila kumtafutia masoko au kumuunganisha wadau wa masoko. Kwa hiyo wamejipanga kuwasaidia Watanzania kwa kuwaunganisha na masoko.

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...