Tuesday, February 23, 2016

WAZIRI KITWANGA NA NAIBU WAKE WAZUNGUMZA NA WATENDAJI WAKUU WA UHAMIAJI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

uha1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini (kushoto) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (kulia), kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Idara hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni. Wakwanza upande wa kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya, na wakwanza upande wa kushoto ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
uha2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akizungumza jambo katika kikao kazi alichokiitisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) kuzungumza na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara yake, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi ndani ya Idara hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni. Wakwanza upande wa kushoto ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
uha3
Kaimu Kamishna wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli (wapili upande wa kushoto) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) kuhusu masuala mbalimbali ya kikazi ndani ya Idara yake katika Kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kilichoitishwa na Waziri Kitwanga na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, balozi Simba Yahya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
uha4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu), Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni (kulia meza kuu) wakifurahi jambo pamoja na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji (kushoto) na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (kulia), wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi ndani ya Idara hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya, na wakwanza upande wa kushoto ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...