Wednesday, February 24, 2016

BENKI YA CRDB YATOA MILIONI 10 KUFANIKISHA MAONYESHO YA WAJASIRIAMALI WANAWAKE ZANZIBAR

Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi ya shs. milioni 10 kwa Mwenyekiti wa Tanzania Informal Sector Foundation ajili ya Maonyesho ya Wajasiriamali Wanawake yatakayofanyika Zanzibar kuanzia Machi 5-8. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Dauda Salmini na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Masudi Maftah.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shs. milioni 10 kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Isiyorasmi Tanzania, Masudi Maftah kwa ajili ya Maonyesho ya Wajasiriamali Wanawake yatakayofanyika Zanzibar kuanzia Machi 5-8. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Mikopo wa CRDB Microfinance, Everson Temu, Mwenyekiti wa Umoja wa Wajasiriamali Wadogowadogo Zanzibar, Nuru Mohamed na Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Dauda Salmini.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wajasiriamali Wadogowadogo Zanzibar, Nuru Mohamed akizungumza baada ya kupokea hundi ya shs. milioni 10 kwa ajili ya ajili ya Maonyesho ya Wajasiriamali Wanawake yatakayofanyika Zanzibar kuanzia Machi 5-8.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wajasiriamali Wadogowadogo Zanzibar, Nuru Mohamed (wa pili kushoto) akipokea hundi ya shs. milioni 10 kwa ajili ya Maonyesho ya Wajasiriamali Wanawake yatakayofanyika Zanzibar kuanzia Machi 5-8, kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa.
 Picha ya Pamoja.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...