Naibu Waziri Dk. Kigwangalla akikagua mahabara ya hospitali hiyo ambayo alikutana na matatizo mbalimbali ikiwemo mashine na vifaa kutotumika ipasavyo na kuagiza uongozi wa kufanya maboresho ndani ya miezi mitatu huku akiahidi kuifungia endapo itashindwa kutekeleza maagizo hayo.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Kigwangalla akiangalia moja ya maeneo ya wodi hizo ambapo alikuta hali ya uchafu pamoja na kuwa na mpangilio mbovu wa namna ya utoaji wa huduma.
Dk. Kigwangalla akitoa maelezo kwa Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Njombe-Kibena, Dk. Samwel Mgema wakati wa maagizo hayo ndani ya siku 90 na endapo hawatafanya utekelezaji ataichukuia hatua ya kuifungia.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Kigwangalla akielekea kwenye baadhi ya majengo ya hospitali hiyo wakati wa ukaguzi huo.
Naibu Waziri wa Afya, Dk Kigwangalla akikagua eneo la kutolea huduma ikiwemo wagonjwa wanaoingia kumuonna Daktari. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Njombe).
Uongozi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe umepewa muda wa siku 90 kurekebisha mapungufu ya utoaji wa huduma za afya, lazima hospitali hiyo itafungwa.
Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na viongozi Mganga Mkuu wa Mkoa, Samwel Mgema na na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Imelda Mwenda na watumishi wa hospitali hiyo.
Dkt. Kigwangalla alitoa agizo kufuatia ziara yake ya ukaguzi wa hospitali, vituo vya afya na zahati ili kuweza kubaini changamoto na mafanikio waliyoyapata baada maagizo mbalimbali kutolewa na Serikali.
Miongoni mwa maagizo hayo ni uboreshaji wa huduma kwa kuwepo na vifaa tiba na vya maabara za kisasa, dawa za kutosha, kuaanza malipo ya mtandao.Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alibaini kwamba hospitali hiyo haina baadhi ya vifaa vya maabara, ambavyo ni muhimu kwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali, ikiwemo mashine ya CT-Scan na kuwepo kwa vifaa vibovu ambayo havijafanyiwa matengenezo, ukiwemo mfumo mbovu wa ukusanyaji taka ngumu na nyepesi.
“Sijaridhishwa na uendeshaji wa hospitali hii na utoaji wa huduma zinazotolewaa ninakuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya, John Luanda kurekebisha mapungufu yaliyopo baada ya miezi mitatu nitarudi nikikuta huduma bado hairidhishi nitakifunga kituo.,” alisema Dkt.Kigwangalla.Aliongeza kuwa akikuta huduma hadhirishi atafunga hospitali hiyo licha ya kuwa ya Serikali, hivyo hatasubiri kutumbuliwa jipu.
Dkt. Kigwangalla aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kuandaa mpango kazi na mkakati wa kuboresha mapungufu yaliyopo katika hospitali hiyo na kuuwasilisha kwake.
Aliutaka uongozi wa hospitali huo kujenga chumba cha upasuaji cha wakina mama na watoto.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Njombe, Mgema alisema watatekeleza maagizo hayo.
No comments:
Post a Comment