Katibu wa Itikadi na Uenezi Mhe. Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM, Ofisi Ndogo Lumumba.
Jana tarehe 07/02/2016 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilikuwa na kikao maalum cha siku moja mjini Dodoma. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho kilikuwa na kazi ya kuteua wagombea wa nafasi mbalimbali zilizo wazi za uongozi ndani ya CCM mikoani na wilayani ambazo uteuzi wake upo kwenye Mamlaka ya Vikao vya Chama Taifa.
Nafasi hizi wazi zimetokana na sababu mbalimbali zikiwemo vifo na baadhi ya viongozi kukihama Chama na kujiunga na vyama vingine. Hivyo, nafasi zilizofanyiwa uteuzi na wagombea wake ni kama ifuatavyo:-
I. UENYEKITI WA CCM MKOA.
1. ARUSHA
(i) Michael Lekule Laizer
(ii) Emanuel Makongoro Lusenga
(iii) John Pallangyo
2. SHINYANGA
(i) Hassan Ramadhani Mwendapole
(ii) Mbala Kashinje Mlolwa
(iii) Erasto Izengo Kwilasa
3. SINGIDA
(i) Hanje Narumba Barnabas
(ii) Misanga Mohamed Hamis
(iii) Mlata Martha Moses
(iv) Kilimba Juma Hassan
II. UJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA NEC
1. NYAMAGANA
(i) DR. Sillinus Elias Nyanda
(ii) Jamal abdul Babu
(iii) Kelebe Bandoma Lutelil
(iv) Patrick Kambarage Nyabugongwe
2. KAHAMA
(i) Pili Yakanuka Izengo
(ii) Paschal Ndibatyo Mayengo
(iii) Sweetbert Charles Nkuba
3. MONDULI
(i) Namelock Edward Sokoine
III. UENYEKITI WA CCM WILAYA
1. MONDULI
(i) Loata Erasto Sanare
2. SUMBAWANGA MJINI
(i) Chami Slegried Mask
(ii) Godfrey Mwimanzi Mwikala
No comments:
Post a Comment