Thursday, February 25, 2016

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MIKOA YA MWANZA, GEITA NA KAGERA

mab01
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akisalimiana na Watumishi wa Hamashauri ya Mji wa Buchosa alipowasili kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi
MAB1
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akipewa maelezo na mtaalam wa mifumo ya uwekaji kumbukumbu za umiliki wa ardhi alipotembelea idara ya ardhi Wilayani Misungwi. Aliyoko katikati ni Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Bw. Mshana.
MAB2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula na Mbunge wa Chato Mhe.Dkt  Medard Kalemani wakikagua eneo la  Kijiji cha Rusungwa lenye mgogoro mkubwa wa ardhi unaofanya wananchi wa kijiji hicho kukosa ardhi ya kulima na uwekaji huduma za jamii kama shule baada ya eneo la ekari 500 la kupewa mwekezaji.
MAB4
Meneja wa NHC Mkoa wa Kagera Bw. Deogratius Batakanwa akimpewa maelekezo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula ya kuhakikisha kuwa anatoa elimu ya kutosha itakayowezesha wananchi, taasisi na Halmashauri ya Muleba kukamilisha ununuzi wa nyumba zilizojengwa na NHC Wilayani Muleba.Naibu Waziri alitembelea nyumba hizo na kulipongeza Shirika la Nyumba kwa ujenzi wa nyumba bora.
MAB5
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akiwa  katika picha ya pamoja na Madiwani wa Halmashauri ya Muleba baada ya kuhutubia Baraza lao na kuliomba liwezeshe ununuzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani humo. Pia aliagiza Baraza hilo kushiriki kikamilifu katika kutatua  migogoro mingi ya ardhi iliyoko katika Wilaya hiyo.
MAB6
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akikagua nyumba zilizojengwa na NHC eneo la Bombambili Mkoani Geita kwa ajili ya kuuza. Amewataka wananchi na Halmashauri ya Mji wa Geita kununua nyumba hizo ili kuliwezesha Shirika kuendelea kujenga nyumba katika Halmashauri zingine.
MAB7
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Mabula akiwa na Mbunge wa Chato Mhe. Dkt Medard Kalemani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini wakikagua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Chato. Katika ziara hiyo Naibu Waziri ameishauri Halmashauri ya Chato kununua nyumba hizo ili NHC iongeze ujenzi wa nyumba zingine kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya nyumba Wilayani humo.
MAB8
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi za NHC Mkoa wa Kagera alipotembelea na kusalimiana na wafanyakazi wa Shirika hilo.
MAB9
Meneja wa NHC Mkoa wa Mwanza Injinia Benedict Kilimba akitoa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Bombambili Geita, kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula alipotembelea mradi huo. Mhe. Naibu Waziri  ameziagiza Halmashauri nchini kusaidia uwekaji wa miundombinu kwenye maeneo ya ujenzi wa nyumba hizo pamoja na kutoa ardhi bure kwa NHC ili nyumba zinazojengwa ziwe na gharama nafuu kwa mnunuzi.
MAB10
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bibi  Mwajuma Nyiruka akitoa taarifa ya sekta ya ardhi ya Wilaya yake kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula alipoitembelea Halmashauri ya Misungwi kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi.
MAB11
Baraza la Madiwani Muleba wakimsikilza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline  Mabula (hayuko pichani) alipohutubia Baraza hilo.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...