Monday, February 22, 2016

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI NA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE IKULU LEO

bal1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bi. Dianna Melrose Ikulu jijini Dar es Salaam.
bal2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Bi. Dianna Melrose Ikulu  jijini Dar es Salaam.
bal3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Mteule wa Namibia hapa nchini Bi Theresia Samaria mara baada ya kupokea Hati ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
bal4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Balozi Mteule wa Namibia hapa nchini Bi Theresia Samaria mara baada ya kupokea Hati ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
bal5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Misri hapa nchini Mohamed Yasser El Shawaf Ikulu jijini Dar es Salaam.
bal6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Misri hapa nchini Mohamed Yasser El Shawaf Ikulu jijini Dar es Salaam.
bal7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Jean Pierre Mutamba Ikulu jijini Dar es Salaam.
bal9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini Thamsanqa Mseleku Ikulu jijini Dar es Salaam.
bal10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU
…………………………………………………………………………………………………….
Uingereza Imempongeza Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Kwa Jitihada Zinazofanywa Na Serikali Yake Katika Ukusanyaji Wa Mapato Na Kukabiliana Na Vitendo Vya Rushwa.
Akizungumza Baada Ya Kukutana Na Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar Es Salaam Leo,Balozi Huyo Mh Dianna Melrose Amesema Juhudi Za Mapambano Dhidi Ya Ufisadi Pamoja Na Kubana Matumizi Na Ubadhirifu Wa Mali Za Umma Kunakotekelezwa Kwa Vitendo Na Serikali Ya Awamu Ya Tano Ni Mfano Wa Kuigwa.
Balozi Melrose Amesema Waziri Mkuu Wa Nchi Ya Uingereza Bw. David Cmeroon Amevutiwa Na Utendaji Kazi Wa Rais Magufuli Na Kusisitiza Kwamba Nchi Hiyo Itaendeleza Ushirikiano Wa Karibu Uliopo Kati Ya Uingereza Na Tanzania Katika Nyanja Mbalimbali Za Maendeleo………………….Mh Dianna Melrose Balozi Wa Uingereza Hapa Nchini
Kabla Ya Kukutana Na Balozi Wa Uingereza Hapa Nchini Rais Magufuli Amekutana Na Kufanya Mazungumzo Na Balozi Wa Afrika Ya Kusini Hapa Nchini Mh Thamsanqa Mseleku,Na Balozi Wa Misri Hapa Nchini Mh Mohamed Yasser El Shawaf Ambao Amewahakikishia Kuwa Serikali Yake Ya Awamu Ya Tano Itaendeleza Ushirikiano Mzuri Uliopo Kati Yake Na Nchi Hizo Hususani Katika Kukuza Biashara Na Kuwanufaisha Wananchi Wa Pande Zote.
Katika Hatua Nyingine Rais Magufuli Amepokea Hati Za Utambulisho Kutoka Kwa Mabalozi Wawili.
Mabalozi Waliokabidhi Hati Zao Za Utambulisho Ikulu Jijini Dar Es Salaam Ni Mh Jean Pierre Mutamba Tshampanga Wa Jamhuri Ya Kidemokrasia Ya Kongo Na Mh Theresia Samaria Wa Namibia.
Rais Magufuli Amewaeleza Mabalozi Hao Kuwa Tanzania Itaendelea kushirikiana Na Nchi Hizo Katika Nyanja Mbalimbali Hususani Katika Uchumi.
Wakati Huo Huo Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Amekutana Na Kufanya Mazungumzo Na Rais Mstaafu Wa Awamu Ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...