Saturday, February 20, 2016

MTANANGE WA YANGA NA SIMBA UWANJA WA TAIFA LEO

 Dakika 90 za Mtanange wa Watani wa Jadi, Simba na Yanga zimemalijika jioni hii hapa uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam kwa kutoka kifua mbele kwa timu ya Yanga baada ya kuchapa Simba bao 2-0. Magoli ya mchezo huo yametiwa kimiani na washambuliaji Donald Ngoma (Dakika ya 38 kipindi cha kwanza) na goli la pili limefungwa na Amissi Tambwe (Dakika ya 34 kipindi cha pili) na kufanya matokeo kubaki hivyo hadi mwisho wa mchezo.PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donald Ngoma (11) akimpiga chenga Golikipa wa Timu ya Simba, Vicent Angban na kupachika bao la kwanza kwa timu yake wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0. 
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Donald Ngoma akishangilia Goli aliloipatia timu yake, wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0. 
Mashabiki wa timu zote mbili waliwa wamefurika kwa wingi ndani ya uwanja wa Taifa.
Golikipa wa Timu ya Simba, Vicent Angban akiwa amejiweka tayari kuokoa mpira uliokuwa ukielekezwa langoni kwake.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Haruna Niyonzima akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya Simba, Kessy Ramadhan, wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0.
Mashabiki wa Yanga baada ya Ushindi.
Mashabiki wa Simba baada ya kuchapwa.




No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...