Sunday, February 07, 2016

PROFESA KILLIAN WA CHUO CHA MKWAWA ASHINDA SAFARI KUTAZAMA BUNDESLIGA UJERUMANI NA STARTIMES


 Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo, akichezesha droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
 Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia) akiandika namba ya mshindi wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo.
 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akipiga namba ya simu ya mshindi aliyepatikana katika droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
 Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo akizungumza na mshindi kwa njia ya simu aliyepatikana wakati wa uchezeshwaji wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Chuo cha Ualimu cha Mkwawa cha mkoani Iringa ambacho ni chuo kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bernadeta Killian (50) amefanikiwa kuibuka mteja wa kwanza mwenye bahati kwa kujinyakulia tiketi ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga kutoka kwa kampuni ya StarTimes katika droo iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza kwa njia ya simu Profesa Killian baada ya kutangazwa kuwa ni mshindi amesema kuwa anayo furaha isiyoelezeka kupata taarifa hiyo ya ushindi ambao hakufikiria kama kuna ofa hiyo nzuri kwa wateja.

“Ninajisikia furaha kwa kutangazwa kuwa mshindi kwani sikutarajia kama wateja wa StarTimes tunaweza kupewa kubwa kiasi hiki ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ‘Live’. Naweza kusema mwaka umeanza vizuri kwa kuonyesha dalili ya neema kama hii, ni fursa kubwa kwangu mimi kama mteja kwani kuna maelefu ya wateja ambao wangependa kupata fursa hii. 

Nawashukuru kwa hili kwani wameliendesha zoezi bila ya upendeleo na sisi wateja wao tunafurahi na kuwapongeza sana na tutandelea kuwaunga mkono.” Alieleza Profesa Killian

Mshindi huyo wa kwanza wa droo iliyopewa jina la ‘Pasua Anga na StarTimes’ alipatikana baada ya kujiunga na kifurushi cha Super ambacho ni shilingi 36,000/- katika dishi. Lakini pia mteja yoyote wa StarTimes anaweza kuibuka mshindi kwa kujiunga na kifurushi chochote kuanzia cha shilingi 5,000/- na kuendelea kwa upande wa ving’amuzi vya dishi na antenna. Na kwa wateja wapya pindi wajiungapo na huduma za kampuni hiyo wamekuwa wameunganishwa moja kwa moja na droo ya bahati nasibu.

“Ningependa kutoa wito kwa wateja wenzangu waendelee kujiunga kwani bado nafasi zimebaki kushindaniwa na zote zipo kwa ajili yao, hivyo wasilaze damu. Ninaahidi kuitumia fursa hii ipasavyo kwa kuenda kutazama wenzetu wa ulaya wanafanya nini kwa upande wa soka kwani kwa muda mrefu tumekuwa tukitazama kupitia kwenye luninga, pongezi tena kwa StarTimes kwa kuifanya ligi ya Bundesliga ionekane kupitia ving’amuzi vyake kwa gharama nafuu kabisa ambayo kila mtu anaweza kuimudu. Wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuipa ligi hiyo umaarufu nchini kwani sasa kwa kiasi kikubwa michezo yote inaonekana ‘Live’ na kufuatiliwa na watu wengi.” alihitimisha Mkuu huyo wa Chuo cha Ualimu Mkwawa

Naye kwa upande wake Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amebainisha kuwa, “Hii si mara ya kwanza sisi kuchezesha droo ya bahati nasibu kwa kuwazawadia wateja wetu ni zawadi mbalimbali, hivyo basi huu ni muendelezo tu wa ofa nyingi zinazoendelea kumiminwa kwa wateja wetu waaminifu. Safari hii wateja wetu tumeamua kuwazawadia safari itakayolipiwa gharama zote na kampuni kwenda Ujerumani kutazama ligi ya Bundesliga ambayo kwa Afrika ndio kampuni pekee yenye hakimiliki ya kuionyesha ‘Live’.”

“Makubaliano baina ya wamiliki wa ligi hiyo ya Ujerumani na kampuni ya StarTimes yaliingiwa kwa dhumuni kubwa la kuifanya ligi hiyo maarufu barani Afrika kama ligi zingine. Na ni kwa kupitia StarTimes pekee hilo linaweza kufanikiwa kutokana na wingi wa wateja wetu, ubora wa huduma na gharama nafuu ambazo mwananchi yoyote wa kipato cha chini anaweza kuzimudu,” alisema Bi. Hanif na kumalizia, “Hivyo basi nampongeza mshindi wa leo na nawasihi wateja wetu waendelee kujiunga nasi au walipie vifurushi vyao ili waingie kwenye droo ya bahati nasibu na kujishindia safari hii kubwa kwenda Ulaya kutazama mechi moja kwa moja pamoja na mashabiki wengine ulimwenguni.”

Akielezea machache kutokana na ushuhuda wake baada ya kupata fursa ya kutembelea ofisi za Bundesliga na kushuhudia mechi kadhaa nchini Ujerumani, Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda, ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli za michezo, amesema kuwa, “Bahati ya kupata safari ya kwenda Ujerumani ni fursa kubwa sana kwa wateja na ningependa waitumie vema. Kuna mengi tu ya kujifunza licha ya kufurahia safari hiyo. Wenzetu wamepiga hatua kubwa na tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwao, hivyo nawasihi waitumie vemam ili waje kutuhadithia na sie huku.”

Zoezi zima la uchezeshwaji wa droo ya bahati nasibu ya kumpata mshindi ilichezeshwa kwa uwazi na haki mbele ya waandishi wa habari ikishuhudiwa na mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

No comments:

TUME YA MADINI YAAINISHA MIPANGO YA KUWAWEZESHA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI

Uanzishwaji wa masoko ya madini wapunguza utoroshwaji wa madini Elimu yatolewa kwa wachimbaji wadogo wa madini CHUNYA Ikiwa ni mkakati wa  k...