Saturday, February 20, 2016

Museveni Ashinda Urais Uganda

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi.

Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu.
Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye alipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.
Awali, waangilizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikuwa wamekosoa uchaguzi huo wakisema kulikuwa na kasoro nyingi.
Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.

No comments:

MALIASILI, MAHAKAMA KUIMARISHA USHIRIKIANO KULINDA HIFADHI

Na Sixmund Begashe, Arusha Wizara ya Maliasili na Utalii imeahidi kuendeleza ushirikiano na taasisi zote zinazounda mnyororo wa haki jinai i...