Monday, February 08, 2016

KIDOGO CHA UCHANGIAJI DAMU CHA MBAGALA RANGI TATU JIJINI DAR CHAZINDULIWA LEO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic akizungumza leo katika uzinduzi wa Kituo cha Damu salama kilichopo Mbagara Rangitatu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadic akikata utepe kuzindua kituo cha uchangiaji Damu salama cha Mbagala langitatu jijini Dar es Salaam leo.
Wananchi wakijitolea damu katika kituo cha Rangi tatu jijini Dar es Salaam leo.
MPANGO wa Taifa wa damu salama nchini ulio chini ya wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto  leo wamezindua kituo kidogo cha uchangiaji damu kilichopo Mbagala Rangi tatu. Uzinduzi huu unaambatana na uzinduzi wa vituo vingine vya afya vilivyopo wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam kama vile Amana, Mwananyama, Sinza, Vijibweni na Mbweni.

Viituo hivi vimejengwa kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali ambao ni Hospitali ya CCBRT, Hospital ya Mbweni Mission MDH, Umoja wa wamiliki hospital binafsi (APHTA) NA Halmashauri za temeke Ilala na Kindondoni.  Vilevile  Mpango wa Taifa wa Damu salama unawapongeza wachangia damu kwa hiari ambao  wamekuwa wakichangia damu mara kwa mara ili kuokoa maisha ya wahitaji tangu kampeni hii ilipoa nza rasmi tarehe 3 februari 2016.

Maisha ya watu wengi yanaokolewa kila mwaka nchini kwa kuongezewa damu . Nchini Tanzania kinamama wengi na watoto hupoteza maisha kwa kukosa damu. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha  kuwa nchini Tanzania takriban wanawake 432 kati ya vizazi hai 100,000 hufa kila mwaka kutokana na uzazi na asilimia 80 ya hivyo vifo husababishwa na ukosefu wa damu. Hivyo ufunguzi wa vituo hivi utasaidia kuondoa tatizo la uhaba wa damu na hatimaye kutokomeza tatizo la vifo vinavyotokana na kukosa damu.

Katika mkoa wa Dare s Salaam mahitaji ya damu ni makubwa , kwa mwezi tunahitaji chupa 4000 lakini zinazopatikana ni chupa 2000 tu ambayo ni nusu ya mahitaji. Kuna wakati mahitaji haya yanakuwa makubwa zaidi na hivyo upungufu huongezeka kufikia asilimia 70, hali ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu.

Damu ni uhai na haipatikani kwa njia yeyote ile isipokuwa  kwa kuchangiwa na binadamu wenzetu . Uchangiaji damu ni zoezi endelevu na la kudumu kwakuwa damu huhifadhiwa kwa muda wa siku 35 tu tangu inatolewa . Kutokana na uhifadhi wa damu kuwa ni wa muda mfupi ndio maana inasisitizwa umuhimu wa watu kuchangia damu walau mara mbili kwa mwaka.




  











No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...