Saturday, February 27, 2016

UCHAGUZI WA MEYA WA JIJI WAAHIRISHWA KWA AMRI YA MAHAKA, POLISI WAPAMBANA NA MADIWANI WA UKAWA


Polisi wakipambana na Madiwani wa UKAWA mara baada ya Uchaguzi huo kuairishwa tena leo kutoka na kesi iliyoko mahakamani iliyofunguliwa(Picha kwa hisani ya Fullhabariblog)
sam2
Mbunge wa Kibamba John Mnyika akiongea na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe kupata ufumbuzi baada ya uchaguzi kuahirishwa kwa amri ya mahakama.
sam3 Polisi wakiwa wamekaa kwenye jukwaa la juu wakifuatilia matukio katika uchaguzi huo ambao umeahirishwa kwa amri ya mahakama.
……………………………………………………………………………………………………………
VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam,mara baada ya uchaguzi huo kuairishwa  tena mwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kwa ajioi ya kutuliza ghasia zilizotokea baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo kutokana nakesi iliyoko mahakamani ambapo Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda  UKAWA walipinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo
Tukio hilo la aina yake limetokea mda huu Jijini Hapa mara baada ya mkurugenzi wa Jiji kutanga kuahirisha uchaguzi huo kwa madai ya uchaguzi huo kusimamishwa na  mahakamani , huku jambo hilo lilowachukiza madiwani wa UKAWA wakidai kuwa hawajapata barua hiyo ya kesi hiyo.
Mara baada ya UKAWA kugomea hoja hiyo ndipo wakafikia hatua ya  ya kutaka kufanya uchaguzi wenyewe huku wakisema akidi ya madiwani kufanya uchaguzi imetimia na wakaomba waendelee kufanya uchaguzi huo, jambo ambalo ni sawa na kukidi amri halali ya mahakama ya kusimamisha uchaguzi huo kutokana na kesi iliyoko mahakamani
Wakati wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo ukawa wenyewe ,ndipo Polisi zaidi ya 15 wakaingia  ukumbini humo na kuwataka  madaiwani   hao waachane na zoezi hilo na kuondoka ukumbini,jambo  ambalo liliwachukiza madiwani hao na kuanza vurugu  ndipo Polisi wakaanza kupambana na madiwani hao wa Ukawa  ili kuwatoa.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...