KAMPUNI ya Sadolin leo imemkabidhi gari aina ya TATA Pic-UP mshindi wa droo ya mwisho ya bahati nasibu iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni hiyo kwa wateja wake wa bidhaa za rangi za aina mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Aliyejishindia gari hilo ni Bi. Monica Benedict Haule mfanyabiashara ndogondogo za uuzaji wa nguo mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam. Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa gari lake Bi. Benedict Haule alisema hakuwa na ndoto ya kumiliki gari maishani mwake lakini leo hii kampuni ya Sadolin wameitimiza ndoto yake.
Akielezea namna alivyoshinda alisema alinunua ndoo mbili za rangi ya sadolin kwa ajili ya kupaka rangi katika nyumba yake na akaelezwa shindano la kukwangua lililokuwa alikiendeshwa na kampuni ya sadolin, kisha akafuata maelekezo na baadae kushinda zawadi hiyo.
“…Siku tegemea katika maisha yangu kwamba siku moja na mimi nitamiliki gari kwa kweli lakini leo hii nimeshinda, namshukuru mungu sana, gari hili sasa litanisaidia katika shughuli zangu na hata kuniingizia kipato,” alieleza Bi. Benedict Haule katika mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake.
Kwa upande wake Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Sadolin, Flora Mapunda alisema mshindi huyo amepatikana baada ya kushinda droo ya mwisho ya Shindano lao la Kwangua na Ushinde na Sadolin lililoanza kuchezeshwa tangu mwezi Machi 2015 kwa nchi nzima kwa wateja wao.
Aidha alisema shindano hilo uchezeshwa kila Mwezi Machi hadi Mwezi Mei ikiwa ni mpango waliojiwekea wa kurudisha sehemu ya faida kwa wananchi na hasa wateja wa kampuni ya Sadolin. Aliwataka wananchi kushiriki bahati nasibu za kampuni hiyo na kutumia bidhaa zao kwani ni za uhakika na wateja hujishindia zawadi mbalimbali kila kinapofika kipindi cha shindano.
No comments:
Post a Comment