Saturday, March 14, 2026

RAIS SAMIA AJUMUIKA NA WANANCHI WETE KWENYE FUTARI YA RAMADHANI PEMBA

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akijumuika na makundi mbalimbali ya Wananchi wa Wete kwenye Futari aliyowaandalia katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Utaani, Mkoa wa Kaskazini Pemba, tarehe 14 Machi, 2026.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kudhihirisha ukaribu wake na wananchi baada ya kujumuika na makundi mbalimbali ya wananchi wa Wete katika futari maalum aliyowaandalia, iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Utaani, Mkoa wa Kaskazini Pemba, tarehe 14 Machi 2026.

Katika tukio hilo lililojaa hali ya upendo, mshikamano na ibada, wananchi kutoka makundi mbalimbali walipata fursa ya kufutari pamoja na Rais huku wakibadilishana mawazo na salamu za Ramadhani. Futari hiyo imeakisi utamaduni wa mshikamano na kuimarisha mahusiano kati ya viongozi na wananchi, hususan katika kipindi hiki kitukufu cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wananchi waliohudhuria walieleza kufurahishwa na kitendo cha Rais kujumuika nao, wakisema hatua hiyo inaonesha kujali na kuthamini mchango wa jamii katika kujenga Taifa lenye umoja na mshikamano. Tukio hilo pia lilikuwa fursa ya kuimarisha maadili ya kijamii, upendo na ushirikiano miongoni mwa Watanzania.






No comments:

RAIS SAMIA AJUMUIKA NA WANANCHI WETE KWENYE FUTARI YA RAMADHANI PEMBA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akijumuika na makundi mbalimbali ya Wananchi wa Wete kwenye F...