Thursday, July 02, 2015

LOWASSA AREJESHA FOMU NA KUONYA WANAOMCHIMBA WAACHE KUENEZA UONGO, ASEMA ANATOSHA KUWA RAIS WA TANO WA JMT

 Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, (kulia), akikabidhi fomu za wadhamini za kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi, (CCM), kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015, kwa Naibnu Katibu Mkuu wa chama hicho, (Tanzania Bara), Rajabu Luhavi, kwenye ofisi za Makao Makuu ya Chama, mjini Dodoma jana Julai 1, 2015. Mh. Lowassa amepata wadhamini mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na jumla ya wana CCM 874,297 wamemdhamini kuwania kiti hicho. 

    WAZIRI Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli mkoani Arusha, Mh. Edward Lowassa, amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu wa 2015. Mh. Lowassa ambaye alikuwa amesindikizwa na Wenyeviti wa CCM wa mikoa 12 kutoka bara na visiwani, aliwasili makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma majira ya saa 8;30 mchana Julai 1, 2015, na kupokewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Rajabu Luhavi. Baada ya kukabidhi fomu hizo, Mh. Lowassa, alikutana na waandishi wa habari na kusoma taarifa yake fupi, ambapo alionya wale wote wanaoeneza habari potofu kuwa yeye ni mla rusha, watoe ushahidi, wapi amekula rushwa, na ni  kiasi gani, za nani na wapi, Awataka Watanzania kupuuza habari hizo na kwani yeye ni muadilifu na hana shaka na hilo. Alisema, yeye ana fedha kiasi gani za kuwapa Wana CCM 874,297, waliojitokeza kumdhamini. "Maneno hayo sasa basi, natoa changamoto kwa yeyote mwenye ushahidi huo autoe hadharani vinginevyo waache kueneza uvumi na uongo" Alisema Mh. Lowassa.  Alisema yeye anachukia umasikini, na kwamba endapo chama kitamteua na hatimaye Watanzania kumchagua kuwa Rais wa awamu ya Tano, atahakikisha anatimiza dhamira yake ya kuwaondolea Watanzania umasikini. Mh. Lowassa, ambaye alisindikizwa na Vigogo wa chama hicho akiwemo, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, na Mzee Pankrans Ndejembi wakiwemo wenyeviti wa CCM 12 kutoka Tanzania Bara na Visiwani, amehitimisha zoezi hilo baada ya kuzunguka mikoa 31 ya Tanzania Bara na Visiwani, na mara zote amekuwa akipata idadi kubwa ya wana CCM na wananchi waliojitokeza kwenye ofisi za CCM mahala alikopita, ikiwa ni pamoja na wengine kujipanga barabarani na kumpungia mikono 
 Mh. Lowassa akilakiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Rajabu Luhavi, kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma jana Julai 1, 2015
 Mh. Lowassa akiwa na Mkewe Mama Regina Lowassa, akiziweka sawa fomu hizo
 Mh. Lowassa, akitoa taarifa fupi mbele ya waandishi wa habari baada ya kurejesha fomu
 Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Geita, Msukuma, akizungumza baada ya Mh. Lowassa kutoa taarifa fupi kwa waandishi wa habari
 Mh. Lowassa, (katikati), akiwa na mkewe Mama Regina, na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, akisoma taarifa hiyo
 Mh. Lowassa akiwapungia wana CCM waliofurika ukumbi wa ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma Julai 1, 2015, baada ya kurejesha fomu
 Mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, Hamisi Mngeja, akizungumza
 Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida
 Mh. Lowassa, akiteta jambo na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru mjini Dodoma
 Mh. Lowassa, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wenyeviti wa CCM wa mikoa wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, mjini Dodoma Julai 1, 2015


 Mh. Lowassa na wenyeviti wa CCM wa mikoa

 Mh. Lowassa akiteta jambo na Mkewe Mama Regina Lowassa
Mh. Lowassa, akipunga mkono wananchi waliofika kwenye ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, wakati akiondoka na gari lake

No comments:

Rais Samia Awasili Dar es Salaam kwa Treni ya Umeme ya SGR Akitokea Dodoma

Dar es Salaam, 22 Januari 2025 – Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili jijini Dar es Salaa...